Facebook watangaza kuingiza utumiaji wa hashtags kwenye mtandao wao maarufu duniani. Hashtags au alama ya reli kwa kiswahili ni mfumo unaotumika katika mitandao mingi ya kijamii kama Twitter, Instagram na Google Plus. Kupitia hashtags watumiaji wataweza kupanga masuala wanayozungumzia na ata pia kuweza kutafuta habari za aina flani kwa urahisi zaidi.
Hichi si kitu cha kwanza Facebook kuingiza kwenye Facebook kutoka kwenye mitandao mingine kama Twitter. Hashtags zilipatia umaarufu kwenye Twitter, mambo mengine ambayo Facebook yalibadilisha ambayo yalitoka Twitter ni pamoja na matumizi ya alama ya “@” kwa ajili ya kutaja watu au kurasa (Pages). Na kiingine ni mabadiliko ya kutoka ‘Subscribe’ kwenda ‘Follow’ kwenye akaunti za watu kama namna nyingine ya uunganishi ukitoa ile ya kuomba urafiki.
Taarifa zilizotoka hadi muda huu ni kuwa utumiaji wa alama ya reli (Hashtags) utakuzwa na kuboreshwa kuwezesha watumiaji kutafuta habari zinazofanana, kushiriki kwenye majadiliano na kama kawaida bilakusahau kuna uwezekano wa Facebook kuongeza mapato ya matangazo kutokana na kutumia mfumo huu.
No Comment! Be the first one.