Kama una marafiki zako ni watumiaji sana wa FourSquare kuna kile kipindi ambacho mmefika bar au hata katika mgahawa na kila mtu anaamua kutoa simu yake na Ku check in. FourSquare wametoa updates katika iOs na Androids na hivyo wameweza kurahisisha zoezi hilo kwa ujumla.
Badala ya kila mtu kutoa simu yake na kuanza kucheck in FourSquare inaruhusu mtu mmoja ku check in kwa ajili ya wote. FourSquare waliandika ‘Kwa wakati mdogo unaotumia katika simu yako, utapata wakati mwingi wa kufurahia sasa’ . Mtu mmoja tuu anaweza toa simu yake na ku check in akisema kuwa yupo na akina nani na nani bila ya wale wenginge kupoteza mda wa ku check in kwa kila mmoja, hii itarahisisha zoezi zima .
FourSquare wamesema kabla ya hapo waligundua kuwa asilimia tisini (90%) za mentions zilikua zikisema nani na nani wapo pamoja kwa mda huo katika updates. Sasa wakati wa ku check in unaweza ukabofya panaposema “I’m With” na hapo utachagua rafiki katika list yako na yeye atapokea request kukubali kua kweli yupo na wewe. kama hatakubali hapo utam ‘mention’ kama kawaida tuu.
FourSquare Wamefanya hivi kwa lengo la kuwafanya watu watumie mda mchache katika simu na kutumia mda mwingi ku ‘enjoy’ na marafiki zao. updates zinapatikana kudownload kwenye Google Play na App Store
No Comment! Be the first one.