Mtandao wa instagram ni moja kati ya mitandao mikubwa sana na inategemewa kwa kiasi kikubwa kama sehemu ya mawasiliano na usambazaji wa taarifa mbalimbali.
Kwa sasa kampuni ya Instagram inakuja na vipengele vitatu vikubwa ambavyo ni Notes ambacho kimeshatoka, Group Profile amabcho kinatoka hivi karibuni na Candid Stories ambacho kipo katika majaribio.
Notes
Kazi kubwa ya Notes ni kumuwezesha mtumiaji wa mtandao wa Instagram kuweza ku’share mawazo yake kwa haraka kwa kutumia maneno na hata emoji.
Notes inahusisha maneno machache sana ambayo yanafikia mpaka maandishi 60 tuu, ukifikiria vifuri unaweza ukasema ni kama Tweet tuu sio? Lakini ni kwamba tuu yenyewe maneno ni machache tuu.
Kingine ni kwamba sio kila mtu anaweza akaona Notes hizi kutokana na jinsi kipengele hiki kilivyowekwa.
Notes zinaweza zikaonekana kwa wale watu –wanaokufuatilia—ambao umewachagua na wale marafiki ambao umewaweka katika orodha ya “Close Friends”.
Notes hizo zitakua zikionekana kwa juu kabisa kwa upande wa DM tuu tena zitakaa hapo kwa muda wa masaa 24 tuu—- yaani kama Story tu na zitaweza kujibiwa kwa njia ya DM pia.
Ili kuelewa zaidi angalia picha hapo chini.
Group Profile
Hapa sasa Instagram inakuja na kipengele kwa ajili ya makundi na hapa ni kwamba makundi hayo yanakua yanapewa Profile kabisa.
Hapa kinachofanyika ni kwamba kundi linakua na ukurasa (profile) lake yenyewe ambapo hapa wanakikundi ndio wanaweza wakawa wanatuma picha na video katika ukurasa huo.
Angalia picha hapo chini ili kuelewa zaidi.
Candid Stories
Hiki pia ni kipengele kipya kabisa katika mtandao wa Instagram na kipengele hiki kitakua kinatumika na wale ambao wamekua wamekiwasha na wanakitumia.
Kipengele hiki kazi yake kubwa ni kutumika katika ku’share kitu ambacho mtu anafanya kwa muda huo, lakini kipengele hiki kama hutaki kukitumia unaweza ukakizima tuu.
Kipengele cha Notes tayari kimeshatoka, kipengele cha Candid Stories kipo katika majaribio wakati kipengele cha Group Profile kinategemewa kutolewa hapo mbeleni.
Kwa sasa hakikisha kuwa una toleo la juu kabia la mtandao wa Instagram ili kuanza kufuruahia baadhi ya vipengele hivi.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Je ushaanza kutumia kipengele cha Notes?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.