fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook Mtandao wa Kijamii Teknolojia

Zaidi Kuhusu Facebook Na Ray-Bans!

Zaidi Kuhusu Facebook Na Ray-Bans!

Spread the love

Unakuambuka niliandika kuhusiana na Facebook kushirikiana na kampuni nguli ya Ray-bans kuja na miwani janja? Unaweza isoma tena –>Hapa<–

Kingine cha kukumbuka ni kwamba habari hiyo ilikua inatupa tuu taarifa juu ya jambo hilo maana kwa wakati huo tulikua hata hatujui kuwa miwani hiyo itakua na vipengele gani.

Vipengele ambavyo vingetupa taswira nzima ya miwani hiyo mpaka tujue kazi yake? lakini kama kawaida kwa haraka haraka nilikua nahisi kuwa bidhaa hiyo itajikita sana katika huduma ya picha na video.

Kwa hilo nilikua sahihi na kwa sasa tuone baadhi ya picha za miwani hiyo

Miwani Ya Facebook Na Ray-Bans

Miwani Ya Facebook Na Ray-Bans

Miwani hii haina tofauti kubwa na ile miwani ya Snapchat ambayo inajulikana kama ‘SPECTACLES’

Miwani Ya Ray-Bans Na Facebook

Miwani Ya Ray-Bans Na Facebook

Miwani hii inajulikana kama Ray-Ban Stories na katika miwani hii ni kwamba kuna kamera mbili kwa mbele ambazo zitakua zikirekodi video na picha

SOMA PIA  Kiwanja cha Ndege cha London kutotumia mtu yeyote katika eneo la kuongozea ndege uwanjani! #Teknolojia

Vile vile kuna kuna kibonyezo juu ya kamera ikiwa ni njia ya kuanza kurekodi au unaweza tuu ukasema “Hey Facebook, take a video” na kuanza kurekodi video

Raybans Kutoka Facebook Na App Ya Kuhariria Picha (Facebook View)

Raybans Kutoka Facebook Na App Ya Kuhariria Picha (Facebook View)

App mbadala ya  Facebook View ndio itakayokuwa ikidaka picha hizo na wewe unaweza anza kuzihariri (edit) picha na video hizo kabla hujazitupia katika mtandao huo wa kijamii.

SOMA PIA  Nokia 3310 (2017) ina Tatizo litakaloifanya kutonunuliwa kwa baadhi ya Nchi #Uchambuzi

Kingine ni kwamba picha na video hizo unaweza hata ukazisambaza katika mitandao mingine ya kijamii ukiachana na mtandao wa Facebook tuu.

Kingine kizuri kuhusiana na miwani hii ni kwamba haina tofauti na miwani ya kawaida kabisa..

Soma Makala Ya Mwanzo Kuhusiana Na Facebook Na RayBans –>Hapa<–

Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Niandikie Hapo Chini Katika Eneo La Comment, Hii Umeipokea Vipi?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

  Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania