Matumizi ya WhatsApp yamekuwa yakishamiri mwaka hadi mwaka na hata watumiaji pia kuzidi kuongezeka siku hadi siku. Vilevile, uwepo wa kipengele cha kutuma jumbe za sauti kwenye WhatsApp imerahisisha mawasiliano ya watu na watu au ndani ya kikundi.
Binafsi nimekuwa mtumiaji wa kipengele cha kuweza kutuma ujumbe ndani ya WhatsApp kwa njia ya WhatsApp lakini mara zote nimekuwa mwangalifu katika kuhakikisha kile ambacho nakituma (katika mfumo wa sauti) hakiendi kuwa changamoto kwa yule anayekipokea.
Marafiki zangu viziwi/wenye usikivu hafifu najua jumbe za sauti kwenye WhatsApp ni kikwazo kwenu hasa kutokana na mlango wa fahamu wenye jukumu la kumuwezesha binadamu/mnyama kusikia kutofanya kazi kabisa katika hali isiyo ya ukamilifu. WhatsApp ambayo inatumiwa na watu wa rika zote imekuwa ikiboreshwa mara kwa mara na sasa kuna hiki ambacho kinatengenezwa:
Kwa mujibu wa WaBetaInfo, WhatsApp inafanyiwa maboresho kwenye kipengele kinachomwezesha mtu kutuma ujumbe katika mfumo wa sauti kuweza kubadilisha na kupeleka katika maandishi.
Kabla ya ujumbe wa sauti kuwa maandishi
Katika kufanikisha adhma ya kubadili ujumbe ullio katika mfumo wa sauti WhatsApp itaomba ruhusa ya kuweza kutambua sauti ya mhusika kwa kuipeleka Apple ambao ndio wenye teknolojia hiyo ya kutambua sauti lakini si kwamba itaweka wazi kwamba hiyo ni sauti fulani.
Nabaki kuwaza tafsiri ya zile ambazo lugha iliyotumika ni Kiswahili tafsiri yake katika maandishi itakujaje 😀 😀 . Basi hatuna budi kusubiri kuona maboresho na daima kumbuka kupakua masasisho ya programu tumishi kwenye simu janja.
Chanzo: WaBetaInfo
2 Comments