fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook Mtandao wa Kijamii

Facebook Kuja Na Miwani Janja Ya Ray-Bans!

Facebook Kuja Na Miwani Janja Ya Ray-Bans!

Spread the love

Facebook licha ya kuwa moja ya mtandao wa kijamii mkubwa na mkongwe sana kwa muda mrefu umekua ukipambana katika kuhakikisha inakuja na bidhaa ambayo inashikika.

Ni kweli tunjaua kuwa Facebook huwa haifanyagi vizuri sana katika aina hizi za bidhaa… licha ya kusema haya unaweza ukashangaa labda pengine ni sababu hawajapata ile bidhaa (umeelewa sio?)

Mfano Wa Miwani Kutoka Ray-Ban

Mfano Wa Miwani Kutoka Ray-Ban

Mkurugenzi mkuu wa Facebook,  Mark Zuckerberg amethibitisha kuwa miwani hizi zinakuja na mtengenezaji ni kampuni maarufu kabisa ya miwani (inaweza kuwa ni kampuni maarufu zaidi katika bidhaa hiyo)

Unaweza ukaanza jiuliza kuwa bidhaa hii itaanza patikana lini, Facebook hawakuongelea juu ya hili lakini fununu nyingi zinasema kuwa bidhaa hii itapatikana muda wowote mwaka huu.

Lakini kwa sasa kwa mtazamo wangu ni kwamba makampuni mengi huwa yanabadilisha ratiba zao kwa kiasi kikubwa sababu ya gonjwa la CORONA.

Kingine cha kuchekesha ni kwamba facebook imesema miwani miwani hii ni mizuri na ukiwa nayo unaweza ukafanya vitu vizuri (nadhifu) lakini ni kwamba hawajasema vitu hivyo.

Mfano Wa Miwani Janja

Mfano Wa Miwani Janja 

Miwani janja hii itakua ni ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya Ray-ban na watakua wanashirikiana na kampuni ya EssilorLuxottica.

SOMA PIA  CHINA: Marekani Inachukua Hatua Nzuri Kwa Kufungulia WeChat Na TikTok!

Kwa haraka haraka mimi binafsi ninavyofikiri ni kwamba miwani hiyo (nadhani) kwa kiasi kikubwa itakua inahusika na mambo ya picha picha na video….

Nahisi unaweza iunganisha na mtandao wao na kuanza kuchukua baadhi ya picha na video ambazo zinaweza zikajipost katika kipengele cha ‘story’ cha Facebook

SOMA PIA  Hili ndio lengo la mmiliki wa Facebook kwa mwaka 2018

Kupata ukweli kamili tusubiria taarifa zenye maelezo ya kina kuhusiana na jambo hili kutoka kwao Facebook wenyewe hivyo tuendelee kusubiri.

Picha Zote Na Chapisho Havihusiani Moja Kwa Moja!

Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Niandikie Hapo Chini Katika Eneo La Comment, Niambia Hii Umeipokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania