fbpx
apps, Facebook, whatsapp

Huduma ya utumaji pesa ndani ya WhatsApp yaanza kupatikana

huduma-ya-utumaji-pesa-ndani-ya-whatsapp-yaanza-kupatikana
Sambaza

Huduma ya utumaji pesa ndani ya app ya WhatsApp yaanza kupatikana nchini Brazili.

Tayari huduma ya utumaji pesa na ufanyaji malipo inapatikana katika Facebook kupitia huduma ya Facebook Pay – inapatikana katika mataifa machache kwa sasa ikiwa ni pamoja na Uingereza na Marekani. Mfumo huu wa malipo katika app ya WhatsApp nao unawezeshwa kupitia teknolojia ya Facebook Pay.

INAYOHUSIANA  Facebook Messenger: Sasa utaweza kupiga simu za makundi (Group Calls)

Kupitia huduma hii ya malipo kwenye app ya WhatsApp mtumiaji ataweza kutuma pesa kwa marafiki na pia kufanya malipo ya huduma kwa biashara zinazotumia huduma ya WhatsApp kwa Biashara (WhatsApp for Business).

utumaji pesa ndani ya WhatsApp yaanza kupatikana
WhatsApp Pay: Utumaji pesa ndani ya WhatsApp

Kutumia huduma hiyo utakuitaji kuingiza taarifa zako za kibenki za huduma za VISA na MasterCard.

Huduma haina makato kwa watumiaji wa kawaida ila wafanyabiashara watakatwa asilimia 3.99 ya malipo yanayofanywa na watu kwenda kwao.

INAYOHUSIANA  CCleaner: Programu muhimu ya kusafisha kompyuta iliyogeuka kuwa kirusi

Je tutegemee huduma hii kutufikia hivi karibuni?

Bado hawajaweka wazi kuhusu usambaaji wa huduma hiyo kwa mataifa mengine. Kwa muda mrefu Facebook wamekuwa nyuma katika kusambaza baadhi ya huduma zake kwenye nchi nyingi zaidi.

Kipaumbele kimekuwa kwenye mataifa yaliyoendelea na mataifa ambayo huduma zake zinawatumiaji wengi sana. Mfano kwa Brazili wana wastani ya watumiaji milioni 120 kwa mwezi kwenye huduma ya Facebook. Hivyo huduma ya Facebook Pay tayari ilikuwa inapatikana katika taifa hilo.

INAYOHUSIANA  Usalama: Hizi ni apps za kuziondoa kwenye simu yako. #Adware #Android #iOS

Tutaendelea kufuatilia maendeleo ya teknolojia hii. Endelea kutembelea TeknoKona.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |