Telegram na Apple yote ni makampuni makubwa sana yanayijihusisha na mambo ya teknolojia. App ya Telegram inapatikana katika soko la Apple maarufu kama AppStore.
Juzi juzi tuliandika kwanini Telegram walitoa lawama kwa Apple, soma zaidi >>HAPA<<
Sababu ya kucheleweshewa kupandishwa kwa sasisho (update) lao ni emoji, Apple wanadai kuwa mtandao wa Telegram umeiga namna ya emoji zao zilivyo.

Kwa sasa toleo hilo jipya (sasisho) limeshatoka na lipo tayari katika AppStore, lakini hili limefanyika baada ya Telegram kuzitoa kwenye App baadhi ya emoji hizo.
Unakumbuka mkuregenzi mkuu wa mtandao huo alikua anasema haelewi kwanini sasisho hilo limekaa katika hatua za ukaguzi kwa wiki mbili nzima bila ya kupewa kibali na Apple? Hii ndio sababu.
Kipengele ambacho kimeleta shida kama nilivyosema ni Emoji na kilikua kimepewa jina kabisa kwa kuitwa ‘Telemoji pack’.
Unaweza ukawa unajiuliza Telemoji ni nini? Bila kupoteza muda, Telemoji ni emoji ambazo zinapatikana katika mtandao wa Telegram tuu.
Ubaya ni kwamba baadhi ya Telemoji zilionekana kama zimetokana na zile emoji za iOS lakini zikaonekana kuwa zimeongezewa mbwembwe tuu katika mtandao huo

Mkurugenzi mkuu wa mtandao wa Telegram amesema licha ya kuwa hilo limetokea, mtandao wake bado utahakikisha kuwa unafanya vitu ambavyo watumiaji wake watafaidika..
…hata kwa Apple kushindwa kuruhusu toleo hilo jipya likiwa na emoji hizo ni swala la ajabu na pengine lingekua na manufaa sana kwa pande zote mbili
Haya bwana, ndio hayo yaliyojiri kwa makampuni hayo mawili, pengine hii unaweza ukaichukulia ni sababu ndogo sana lakini kwa makampuni kama haya huwa hakuna sababu ndogo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Ulidhani sababu ya yote haya inaweza ikawa ni emoji?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.