Usiku wa jana huku kwetu kwa huko nchini Marekani jijini San Francisco ilikuwa ni muda ambao kampuni ya Apple ilikuwa inafanya kitu ambacho huwa inafanya takribani mara mbili kwa mwaka. Ilikuwa inatambulisha vitu vipya, na kwa kiasi kikubwa ni kwa mara ya kwanza imeweza kuleta mabadiliko makubwa katika sehemu flani flani katika bidhaa zake.
Je ni mambo gani hasa unatakiwa kujua?
MacBook Air zenye uwezo wa kukaa na charge masaa 12!
Sahau tableti, kwa kutumia ‘chip’ mpya za aina ya Hanswell kutoka kampuni ya Intel Apple wameweza tengeneza laptop zenye uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa masaa 12 baada ya kuichaji mara moja.
The new 13″ MacBook Air ya inchi 13 ndio itakuwa na uwezo huo wakati ile ya inchi 11 itaweza kukaa hadi kwa muda wa masaa 9 baada ya kuchajiwa mara moja.
Bei ya MacBook Air ya inchi 13 itakuwa inaanzia Dola za Kimarekani $1,099 (Takribani Tsh 1,796,865/= ) wakati ile ya inchi 11 itaanzia dola $999 (Takribani Tsh 1,633,365/=).
MAC OS X Mavericks
Ndiyo jina lililopewa kwa toleo jipya la programu ya uendeshaji wa kompyuta za Apple (Mac). Baadhi ya mabadiliko ya muhimu yaliyokuja ni pamoja na uwezo wa kupanga mafolda,na mafaili kwa kuziwekea lebo (‘tags’), na programu hii inakuwa na tofauti ya takribani asilimia 28 ya uzito wa utendaji (CPU).
Safari Browser
Safari Browser imepata vitu vipya. Kwa sasa inakuwa na muunganisho wa moja kwa moja na huduma za Twitter na LinkedIn, hivyo kukuwezesha kusoma habari kutoka mitandao hiyo ya kijamii haraka zaidi. Pia imekuwa na mwendo kasi wa utendaji mkubwa zaidi.
Pia kwenye mkutano huu walitambulisha MacBook Pro mpya, lakini kitu kingine kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa kwa hamu ni toleo jipya la programu ya uendeshaji wa simu za iPhone na tableti za iPad.
iOS 7: Mabadiliko Makubwa Tokeo Simu ya Kwanza ya iPhone Itoke!
Ndio, mabadiliko ya kimuonekano katika toleo hili ni makubwa sana. Hii imetokana na msukumo kutoka kwawatumiaji wa muda mrefu waliokuwa wanaona hakuna jipya kwenye mvuto wa mtazamo ukilanganisha na ule wa Android. Na hakika Apple imefanya kileambacho kilikuwa kinategemewa kwa sana.
Muonekano wa iOS 7 |
iOS 7 ina sura mpya. Rangi na muonekano wa aikoni (icons) umefanyiwa mabadiliko. Kwa sasa muonekano unavutia na hakika unaonekana ni wa kisasa.
Safari Browser imeboreshwa na sasa itakuwa inakuwa fullscreen, sehemu nyingine palipo guswa ni pamoja na kuweka ‘effects’ katika tabia ya ‘wallpaper’. Pia Game Centre imefanyiwa maboresho ya kimtazamo, na sasa wengi wanasema ndio inavutia zaidi.
App ya ‘Photo'(Picha) kwa sasa itakuwa inakusaidia kupanga picha zako vizuri zaidi, na hii ni pamoja na kuongezwa kwa uwezo wa kutuma kwa uraisi zaidi picha zako kwenda mitandao ya kijamii.
Kingine ni kuwa sahau kuhusu kuwa na taarifa (notifications) kuhusu apps mia au hamsini zinazohitaji kupandishwa toleo kwenda matoleo mapya zaidi (updates), kwa sasa kutakuwa na ‘auto-update’, yaani apps zitakuwa zinajipandisha toleo zenyewe. Usihofu suala la kifurushi chako cha intaneti kwani zitafanya hivyo ukiwa umeunganishwa kwenye intaneti ya bila waya (wireless/wi-fi). Na pia apps kubwa kama gemu la Asphalt na mengine yenye ukubwa mkubwa sana yatafanya hivyo ukiwa umechomeka kifaa chako kwenye chaji pia.
Hayo ndo baadhi mambo muhimu ya kujua kuhusu kipya kutoka Apple, tutegemee iOS 7 kuwa tayari kwa watumiaji wote ndani ya miezi michache baadae.
No Comment! Be the first one.