fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta Sayansi Teknolojia Windows 8

VivoMouse: ASUS Yazindua Mausi Kwa Ajili Ya Windows 8 !

Spread the love

ASUS yazindua mausi hiyo ambayo inasemekana kuwa ni ya kwanza kwa dunia ambayo ni  ‘MultiTouch  Vivo Mouse’ spesho kwa ajili ya Windows 8.  Mouse hii haina vibonyezo kabisa hivyo imefanya kuwa ya kwanza kua na Tachi padi zilizojengewa vyema  ndani hivyo unaweza gusa upande wa kulia au wa kushoto mwa duara kama mouse nyingine jinsi unavyo ‘click’.  

Pia haina waya ambao unaiunganisha na kompyuta. Licha ya kwamba watumiaji wengi wa windows 8 hawahitaji sana mouse ya nje lakini wanahitaji ku ‘click’ . Ndio unaweza tumia padi ya mguso (touch pad) ya ‘VivoMouse’ kukuza na ku’scroll’ chini au juu. Katika maonyesho ya Computex nchini Taiwan ndipo ASUS walipozindua VivoMouse.

Kama VivoMouse ikiwa ni bei rahisi ASUS inaweza ikauza sana kutokana na uwezo tofauti wa VivoMouse na pia urahisi unaletwa na kifaa hichi. Japokuwa kwa sasa ASUS bado hawajaweka wazi bei ya mausi hiyo na ninashaka kama itakua bei rahisi. VivoMouse itaenda kwenye mauzo mwaka huu 2013 muda wowote katika miezi michache ijayo.


Kwa hiyo tutegemee mambo mengi mapya kwa watengenezaji na wataalamu wa masuala ya Kompyuta  huko barani Asia katika kipindi kidogo cha muda kijacho!

SOMA PIA  Kipya kwenye WhatsApp: Angalia picha/video mara moja tu!
Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania