fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
simu Smartphones Tecno Teknolojia

TECNO CAMON 18 Kuja Na ‘GIMBAL’ Kamera!

TECNO CAMON 18 Kuja Na ‘GIMBAL’ Kamera!
Spread the love

Kuelekea mwisho wa mwaka 2021 kampuni ya simu za mkononi TECNO yenye mashabiki wengi hasa upande wa simu janja inatarajiwa kuzindua ….

…toleo jipya la mfululizo wa simu zake aina ya TECNO Camon 18 yenye ubora ulioboreshwa hasa upande wa picha na video.

TECNO CAMON 18

TECNO CAMON 18

Matoleo ya CAMON imekuwa ikiaminika kuwa na simu zenye kamera kali kutoka kwenye kampuni hiyo, japo simu hiyo haijatambulishwa rasmi lakini tayari kuna tetesi huenda simu hiyo ni TECNO Camon 18.

SOMA PIA  Obama na mkewe wapo kwenye mazungumzo na Netflix, kuja na Shows

TECNO Camon 18 inasemekana kuja kuwa suluhisho kwa wenye uhitaji mkubwa wa kamera katika kazi za kila siku hata kwa waandishi wa habari itawasaidia katika kuchukua matukio kadha wa kadha ambapo ina Mega Pixel 64.

Simu hii inayosemekana kuwa camon 18 ndiyo simu ya kwanza TECNO kuwa na GIMBAL CAMERA hii ni kamera ya hali ya juu sana katika mfumo mzima wa uchukuaji video kuwahi kutokea TECNO ambapo inaweza kurekodi video HD katika mazingira yoyote yale hata kama mchukuaji video anakimbia au kutembea lakini video haitotingishika.

TECNO CAMON 18 GIMBAL CAMERA

TECNO CAMON 18 GIMBAL CAMERA

Pia simu hii ya CAMON 18 ina kamera yenye uwezo mkubwa wa ku-zoom mara 60X Zaidi na kufanya kitu kilichokuwa mbali na kuwa karibu Zaidi. Bila kusahau main kamera ya CAMON 18 ina mega pixels zipatazo 64 za kukuwezesha kupiga picha safi katika mazingira ya usiku na mchana.

Muonekano Wa Gimbal Camera Katika Comon 18 Kutoka TECNO

Muonekano Wa Gimbal Camera Katika Comon 18 Kutoka TECNO

Pia wameboresha uwezo wa kuhifadhia kumbukumbu ni mkubwa zaidi ambapo itakuwa na 256GB ROM kwa 8GB RAM hivyo kuzidi kumvutia mteja kumiliki simu hii yenye uwezo mkubwa zaidi. Kufahamu Zaidi kuhusiana na CAMON 18 tembelea @tecnomobiletanzania

SOMA PIA  Facebook yalegeza masharti kuhusu matangazo ya sarafu za kidijitali

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, hii umeipokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia.

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania