fbpx

Unamfuatilia kisiri mtu Instagram? Instagram wafanya iwe vigumu!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Kama unamfuatilia kisiri mtu kwenye app ya Instagram basi fahamu mabadiliko yanayokuja kwenye app hiyo yatazidi kuifanya kazi hiyo kuwa ngumu.

Kwa muda mrefu kuna eneo la kwenye app hiyo linalotambulika kama ‘Following tab’, ni ene ambalo limekuwa likikupa taarifa kuhusu mambo yanayofanywa na wale unaowafuata. Mfano kama marafiki zako kadhaa wameLike au kucomment sehemu basi Instagram ilikuwa inachagua kukupa taarifa kulingana na jinsi gani unawafuatilia sana au kuchati na watu hao sana.

kumfuatilia mtu kwenye instagram

ZAMANI: Ulikuwa unaona taarifa zinazokuhusu na taarifa kuhusu mambo yanayofanywa na marafiki zako (watu unaowa’follow

kumfuatilia kisiri mtu instagram

SASA HIVI: Eneo linaloondoka kwenye Instagram. Hautaona tena taarifa kuhusu wengine wamefanya nini, utaona taarifa zinazokuhusu tuu.

Sehemu hii imekuwa ni kikwazo kwa wengine, hasa hasa wanakuwa na wasiwasi kuhusu mambo yao mengine wanayoyafanya hasa hasa kwenye kulike picha ambazo mtu au watu wanaowafollow wakipewa taarifa zitawaingiza kwenye matatizo.

Mfano:

Mtu anaweza akawa amelike picha ya mpenzi wake wa zamani na Instagram wakampa taarifa mpenzi mpya kwenye eneo la Following Tab kwamba ‘Bwana XYZ amelike picha ya YYZ’, jambo kama hili linaweza leta matatizo kwa watumiaji wengi.

Mfano mwingine ni pale ambapo mtu haukujibu au haujibu ujumbe wa mtu mwingine kwa kigezo upo bize sana…alafu huyo mtu mwingine apate taarifa zako unapiga likes na una comment Instagram kwa sana kwa muda huo.

Ingawa Instagram wametangaza rasmi utolewaji wa eneo hilo wiki hii tayari kuna baadhi ya watumiaji walishaanza kukosa kuona eneo hilo tokea mwezi wa nane. Inaonekana Instagram walianza kufanya kama majaribio uondoaji wake.

INAYOHUSIANA  Jifunze kutengeneza mafaili ya GIF kupitia WhatsApp

Kwa wanaotumia matoleo ya kisasa ya Instagram msishangae mkikuta eneo hilo halipo tena. Je una mtazamo gani juu ya uamuzi huu? Tuambie kwenye comment.

Vyanzo :Techcrunch na vyanzo mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.