fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Facebook instagram Intaneti

Instagram yamfungia ndugu wa Hayati Rais John F Kennedy kwa taarifa za uongo juu ya Covid-19

Instagram yamfungia ndugu wa Hayati Rais John F Kennedy kwa taarifa za uongo juu ya Covid-19

Spread the love

Instagram yamfungia ndugu wa aliyekuwa Rais wa Marekani, John F Kennedy kutokana na kusambaza taarifa zisizokuwa sahihi kuhusu maambukizi ya Covid-19.

Instagram yamfungia ndugu

Instagram yamfungia ndugu wa Hayati Rais John F Kennedy kwa taarifa za uongo juu ya Covid-19, Bwana Robert F. Kennedy Jr

 

Bwana Robert F. Kennedy Jr ni mpwa wa aliyekuwa Rais wa Marekani, ambaye ni maarufu pia kutokana na kuuliwa kwa shambulio la risasi. Rais John F Kennedy alikuwa rais wa wa Marekani.

SOMA PIA  Ericsson Wapata Mkataba Mnono Kutoka Kampuni ya Smile

Kwa kipindi kirefu Bwana Robert F. Kennedy Jr ambaye ni mwanasheria na mwanamazingira amekuwa akipost habari ambazo zinatuhumiwa kuwa hazina ukweli wowote juu ya janga hilo. Amekuwa akipinga vikali utumiaji wa chanjo za Covid19 na kuzungumza mengi ambayo serikali na watu wengine wamekuwa kuyapinga wakisema hayana ukweli wowote.

Facebook wamesema wataendelea kuchukua hatua kali dhidi ya akaunti zozote Instagram au Facebook zitakazokuwa zinatuma jumbe ambazo si zahihi kuhusiana na janga la Covid 19.

Suala hili kufungia akaunti kutokana na misimamo yao limeanza kuwa gumzo hasa baada ya Twitter, Facebook, Instagram na wengine kufunga akaunti za aliyekuwa Rais wa Marekani, Bwana Trump. Je suala hili haliingilii suala la uhuru wa maoni? Kama wametenda kosa – kushitakiwa sio ndio njia sahihi kuliko kuondoa akaunti zao? Tuambie maoni yako.

Chanzo: TheVerge na Facebook

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania