Gharama za mawasiliano ni moja ya sababu ambazo zinawafanya watu kuhama/kuwa na kadi za simu kutoka mitandao tofauti tofauti na mwisho wa siku unakuwepo ushindani kuhakikisha kila mtu anavutia wateja kwa namna yake.
Airtel Tanzania imekuwa ikitoa huduma za mawasiliano mijini na vijini kwa miaka mingi sasa na imekuwa ikipata ushindani mkali kutoka kwa Voda, Tigo na hivi karibuni Halotel. Sasa basi daima haya makamuni yanafikiria namna ambavyo itawashawishi iendelee kubaki na wateja wake, kupata wateja wapya mwisho wa yote kupata faida kubwa zaidi.
Sasa basi, mtandao unaotoa huduma za mawasiliano, Airtel Tanzania kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Masoko kutoka kampuni hiyo kuwa gharama za mawasiliano kupitia mtandao huo zimepungua kwa 80% ambapo hivi sasa kupiga simu Airtel-Airel au Airtel kwenda mitandao mingine ni Tsh. 1/sekunde tofauti na awali ilikuwa inagharimu Tsh. 5/sekunde (Airtel-Airtel) au Tsh. 7.6/sekunde (Airtel-Mitandao mingine).
Hapo awali ilikuwa ukiweka vocha ya Tsh. 500 na ukapiga simu bila kuunganisha kifurushi mteja aliweza kuongea kwa nakika moja na nusu lakini hivi sasa mteja ataweza kwa dakika nne. Tozo ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi ni Tsh. 10 kutoka Tsh. 50. Kifurushi cha intaneti (MB 1) ilikuwa ni Tsh. 172 na hivi sasa ni Tsh. 40.
Airtel Tanzania yapunguza gharama za kufanya mwasiliano.
Hatua hiyo muhimu sio ya muda mfupi (kuwa na ukomo) la hasha! Bali ni mabadiliko ambayo kampuni husika imeyafanya kutokana na malamiko ya muda mrefu kutoka kwa wateja wao. Tuambie, umefurahishwa na habari hii?
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|