fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Motorola simu Teknolojia

Ingizo jipya la simu janja Motorola One 5G UWB Ace

Ingizo jipya la simu janja Motorola One 5G UWB Ace

Spread the love

Makampuni mengi yanaweka nguvu nyingi kwenye teknolojia iliyoshika hatamu katika miaka ya karibuni. Kwenye simu janja 3-5 zinazotoka basi mojawapo utakuta ni ya 5G kama Motorola One 5G UWB Ace.

Motorola imendelea kujiweka vizuri kwenye soko la 5G ambapo mwezi Januari mwaka huu ilitoka Motorola One 5G Ace na miezi kadhaa baadae (Julai 2021) imetoka Motorola One 5G UWB Ace. Simu hii ambayo ina sifa hizi:

Memori :
 • Diski uhifadhi: 64GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada mpaka TB 1
 • RAM: GB 4
Kamera :
 • Kamera Kuu: MP 48, 8 na 2+taa moja ya kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu. Ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 4K na 1080px
 • Kamera ya Mbele: MP 16+uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 1080px
  Motorola One 5G

  Inavyoonekana Motorola One 5G UW ACE upande wa mbele/nyuma na mpangilio wa kamera kwa pande zote mbili.

   

Betri/Chaji :
 • Li-Ion 5000 mAh
 • USB-C 2.0, OTG+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 20W
Kipuri mama :
 • Snapdragon 750G 5G

Programu Endeshi

 • Android 11
Rangi/Bei :
 • Kahawia
 • GB 4/64-$299 (zaidi ya Tsh. 687,700) bei ya ughaibuni
  Motorola One 5G

  Ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, inatumia kadi mbili za simu, mnara wa mawasiliano ni GSM / HSPA / LTE / 5G, Bluetooth 5.1, WiFi, NFC.

   

Kwa wale ambao tunapenda simu janja ya uwezo wa kati na nzuri kwenye ulimwengu wa 5G hili litakuwa ni chaguo zuri na bora zaidi iwapo utalinganisha na toleo lililotoka mwezi Januari mwaka huu.

Vyanzo: Gadgets 360, News 18

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania