fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Unafahamu sifa za simu janja Samsung Galaxy A52?

Unafahamu sifa za simu janja Samsung Galaxy A52?

Spread the love

Samsung wana simu lukuki sokoni na wamekuwa wakitoa toleo moja baada ya jingine zikiwa zinapishana muda mfupi tuu na mapema mwaka huu walizindua Samsung Galaxy A52 ambayo inaonekana kuwa ni kivutio cha wengi.

Kama mdau wa masuala ya teknolojia simu hii imenivutia kwa namna yake hasa ukizingatia soko la ushindani lina rununu kedekede kiasi kwamba inakuwa vigumu kwa watu kuweza kuamua wanunue ipi kwa wakati ambao wanahitaji simu janja. Sifa za simu hii ni kama ifuatavyo:-

Memori :
 • Diski uhifadhi: 128GB/256GB
 • RAM: GB 4/6/8
Kamera :
 • Kamera Kuu: MP 64, 12, 5 na 5+taa moja ya kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu. Ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 4K na 1080px
 • Kamera ya Mbele: MP 32+uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 4K na 1080px
  Galaxy A52

  Samsung Galaxy A52: Muonekano wa nyuma na mpangilio wa kamera. Upnde wa mbele unalindwa na Gorilla Glass 5.

   

Betri/Chaji :
 • Li-Ion 4500 mAh
 • USB-C 2.0, OTG+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 25W (50% ndani ya dakika 30 tu)
Kipuri mama :
 • Snapdragon 720G
Uzito :
 • Gramu 189

Programu Endeshi

 • UI 3.1, Android 11
Rangi/Bei :
 • Nyeusi, Nyeupe, Zambarau na Bluu
 • Gharama yake inaanzia $443 (zaidi ya Tsh. 1,018,900) bei ya ughaibuni
  Galaxy A52

  Simu hii ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, inatumia kadi moja/mbili za simu, teknolojia ya kutumia alama ya kidole imewekwa chini ya kioo, mnara wa mawasiliano ni GSM / HSPA / LTE, Bluetooth 5.0, WiFi, NFC.

   

Samsung wameamua kutuletea vizuri. TeknoKona hatuna mengi zaidi ya kukuachia wewe uweze kufanya maamuzi ya kuipata au la!. Endelea kukaa nasi kwa habari mbalimbali za teknolojia kila siku.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

 1. […] Simu janja za Samsung  zimeendelea kuongezeka ambapo takribani wiki mbili zilizopita Galaxy A52s 5G ilizinduliwa ikiwa tayari kwa wale wanaopenda kupata raha ya 5G. […]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania