fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple iOS IPhone

Jinsi Ya Kujua Apps Unazozitumia Sana Katika iPhone! #iOS #ScreenTime

Jinsi Ya Kujua Apps Unazozitumia Sana Katika iPhone! #iOS #ScreenTime

Spread the love

Hivi ushawahi kujiuliza kwamba ni App zipi katika iPhone yako unazitumia sana? sawa inawezekana kwa harahara ukajiua kwa kuangalia uliyotumia sana.

Lakini je unaweza jua hata kwa kipindi cha wiki moja umetumia muda gani katika hizo App? hapo kidogo itakua ni shida sio?

Katika simu za iPhone kipengele hicho kinajulikana kama ‘Screen Time’ na ili kupata huduma hii inakubidi uhakikishe umekiwasha.

iPhone 11

iPhone 11

Jinsi Ya Kuwasha.

  1. Nenda Settings > Screen Time.
  2. Ingia Turn On Screen Time.
  3. Ingia Continue.
  4. Chagua ‘This is My [device]’ au ‘This is My Child’s [device]’
SOMA PIA  Uwezo wa kuficha utambulisho wa kiongozi wa kundi kwenye Telegram

Baada ya hapo utakua umeshawasha ‘Screen Time’ na ukitaka kujua muda ambao umetumia kwa App mbalimbali katika iPhone  yako inakubidi uende katika settings na kisha uende katika ‘Screen Time’.

List Ya App Ndani Ya 'Screen Time'

List Ya App Ndani Ya ‘Screen Time’

Kingine kikubwa hapa inabidi muda kidogo upite ila App ikusanye taarifa za msingi.. maana huwezi kuwasha tuu na yenyewe ikaanza kukupa taarifa za App unazotumia sana (kama ilikua imezimwa).

SOMA PIA  Mac Pro iliyoboreshwa na yenye nguvu zaidi kutoka Apple

Ukifanikiwa kuingia kuna mengi uaweza fanya maana utakua unapata taarifa nyingi za App zako. Pia unaweza ingia ndani na kuanza kuhariri App moja moja na kuifanyia uhariri

Muonekano Kama Ukiinga Ndani Ya App Moja Moja

Muonekano Kama Ukiinga Ndani Ya App Moja Moja

Ukiingia ndani ya Add Limit kupitia app yeyote hapo unaweza ukaongeza au kupunguza muda wa kutumia App hii jinsi unavyotaka wewe.

SOMA PIA  AirPlay kuwekwa kwenye VLC Player

Kama utakuwa umepanga kabisa kwamba App fulani itumie muda wako (fulani) basi itakupa taarifa (notification) pale muda wako wa kutumia App hiyo unavyokaribia kuisha.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niambie hii umeipokeaje? hii ni nzuri sana katika kuhakikisha jambo la kupambana na uraibu wa kutumia simu janja, maana ni wazi simu zetu zinakula sana muda wetu kwa siku.

Niandikie Hapo Chini Katika Eneo La Comment. Pia Kumbuka Kutemebelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania