Ngoja kwanza sio kila anaetumia akaunti ya kawaida tuu ya kwa sasa nazungumzia watumaiji wa huduma ya youtube ile ya kulipia yaani Youtube Premium.
Kinachotokea hapa ni kwammba huduma hii kwa sasa inapatikana katika huduma ya Youtube Premium na hii ni mpaka kufikia tarehe 1 septemba.

Yaani huduma hii baada ya septemba sasa itakua ni juu ya kampuni ya Youtube kama itaamua kuendelea nayo katika huduma yake ya Premium au itaamua kuachia kwa watumiaji mpaka wale wa Youtube ya kawaida.
Lakini ukiachana na hayo hata hivyo mtandao unaweza ukaamua kuachana kabisa na huduma hiyo….kwa kifupi ni jinsi kampuni yenyewe itakavyo amua.
Kwa sasa unaweza Ku’zoom video mbali mbali katika Youtube Premium kwa kutumia vidole viwili vya mikono yako.
Njia hii ya ku’zoom ni ya kawaida kabisa na imezoeleka sana kwa watu mbali mbali hata katika video za kawaida ambazo ziko katika simu janja zetu.

Kwa sasa ni kwamba huduma hii ipo katika kipindi cha majaribio mpaka kufikia septemba 1 mwaka huu.
Kaa ukijua kama kwa sasa unataka kuanza kutumia huduma hii ni lazima uwe na huduma ya Premium, na kwa sasa watumiaji wa huduma hii ndio wenye hata uwezo wa kutoa mrejesho jinsi huduma hii ilivyo katika Google.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani hii ni hatua nzuri kutoka kwa mtandao huu? Je uko tayari kuanza kuzoom katika video za Youtube?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.