Huduma ya ‘picture in picture’ ni ile ambayo inakuwezesha kuweza kuangalia video huku unafanya vitu vingine katika kifaa chako.
Tulishagusia kuhusiana na huduma hii ya picture-in-picture >>HAPA<< soma tena kujua Zaidi.
Sasa unaweza kuangalia video za youtube kwenye kiboksi kidogo ambacho kinaenlea katika uso wa kifaa chako wakati unafanya mambo mengine katika simu yako ya iPhone.
Cha kufnaya ili kuwezesha hili inakubidi uingie katika eneo la ‘Settings’ katika simu yako ya iPhone
Nenda katika eneo la General
Chagua ‘Picture in Picture’
Kisha hakikisha umewasha sehemu ya ‘Start PiP Automatically’
Ukishafanikisha hilo utakua umeshawezesha utumiaji wa huduma hiyo, kwa mfano ukiingia katika mtandao wa Youtube baada ya kuwezesha hili..
Kutumia iPhone yako (matoleo ya juu) unaweza kufanya kama vile unaenda katika uso wa nyumbani (home screen) na hapo video hiyo itajitenga katika koboksi kidogo huku simu ikikupeleka katika eneo la nyumbani (Home) ili uweze kutumia simu yako kwa kufanya kitu kingine kama vile kutuma meseji n.k.
Una uwezo wa kuzima kabisa video hiyo wakati ikiwa bado inajicheza katika kiboksi hiko kidogo wakati ukiwa unafanya mambo mengine katika simu yako kwa kuchagua kialama cha X.
Ukichana na kuifunga tuu unaweza amua kurudi kabisa katika App ya Youtube na kuendelea kuangalizia video yako kule.
Kwa sasa huduma hii inapatikana kwa watumiajia wa Youtube huko marekani na maeneo mengine machache tuu lakini hapo baadae itaanza kutumika kwa watumiaji wote.
Kingine ni kwamba watu ambao wanatumia App ya youtube ya kawaida wana uwezo wa kutumia huduma hii kwa zile video ambazo sio za muziki.
Watumiaji wa Youtube Premium wana uwezo wa kutumia huduma hii kwa video za aina zote yaani zile za video za muziki na zile ambazo sio.
Ningependa kusikia kutoka kwako, nandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Unakumbuka ile kero ya kuwa Youtube alaf unataka kufanya kitu kingine katika simu yako ni lazima utoke katika App hiyo?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.