fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Barua pepe Microsoft

Outlook Lite Hii Hapa, Ni 5MB Tuu Kwa Ajili Ya Android!

Outlook Lite Hii Hapa, Ni 5MB Tuu Kwa Ajili Ya Android!

Spread the love

App hii ya Outlook Lite ni mahususi kwa simu za Android ambazo zinatumia hazina uwezo mkubwa au zina matumizi madogo ya intaneti.

Wakati App hii, Outlook Lite  imetangazwa kama iko njiani kuja tuliandika kuhusu jambo hilo >>HAPA<< hebu pitia tena.

App ya Outlook Ya Mfumo Wa Lite

App ya Outlook Ya Mfumo Wa Lite

Hapa hakuna kitu cha kushangaza sana kwani App hii ni kama App ile ya kawaida kabisa ya Outlook tuliyoizea tuu lakini hii ina ujazo mdogo na ni nyepesi Zaidi kulinganisha na ile tuliyoizoea.

App hii itakua ikiruhusu barua pepe (email) za akaunti Microsoft kama vile Outlook.com, Hotmail, Live,MSN, Microsoft 365 na hata Microsoft Exchange Online.

Ukiachana na hii ni kwamba App hii itakua haisapoti barua pepe zile za nje na mfumo wa Microsoft yaani kama vile Gmail na nyinginie nyingi.

Outlook Lite

Outlook Lite

Kizuri kuhisiana na App hii ni kwamba inafanya kazi vizuri sana hata katika simu zenyeuwezo wa 3G na 2G bila tatizo lolote

SOMA PIA  Microsoft Office 2021 inakuja kwa Windows na MacOS mwaka huu

Kwa Sasa App Hii Inapatkana Katika Maeneo Ya.

 • Argentina
 • Brazil
 • Chile
 • Colombia
 • Ecuador
 • India
 • Mexico
 • Peru
 • Saudi Arabia
 • South Africa
 • Taiwan
 • Thailand
 • Turkey
 • Venezuela

Hapo mbeleni kuna uwezekano mkubwa wa huduma hii ya Outlook Lite kumfikia kila mtu duniani kote na kama inavyojulikana kwa sasa huduma hii inapatikana katika vifaa vya Android Pekee.

Outlook Lite Katika Android

Outlook Lite Katika Android

Outlook  ni moja kati ya majukwaa makubwa kabisa katika maswala ya kutuma barua pepe na kupangilia vitu mbalimbali kwa kutumia kalenda.

SOMA PIA  Njia Za Kujilinda Na Kuepuka Kupokea Barua Pepe (E-mail) Za Spam!

Ningependa  kusikia kutoka kwako, hebu niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Unaweza kuwa unatumia huduma hii ?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hash

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania