Xiaomi waamua kufungua ukurasa mpya na kuanzisha biashara mpya ambayo inaonekana kuendelea kupata soko kutokana na ukuaji wa teknolojia kwenye magari yanayotumia nishati ya umeme.
Ktika hatua ya kutanua wigo wa biashara na kufikia wateja wapya kwenye biashara ambayo ndio mara yao ya kwanza kuifanya Xiaomi wamesajili kampuni mpya iitwayo Xiaomi EV Inc. mahususi kabisa kwa ajili ya biasharta ya mgari ambayo yanatumia nishati ya umeme.
Katika kusisitiza hilo hivi karibuni Xiaomi wamenunua kampuni iitwayo DeepMotion amabayo imejikita kwennye teknolojia ya magari yanayojiendesha yenyewe. Ktika kipindi cha miezi mitano Xiaomi wamewekeza $1.5 bilioni pamoja na kuajiri wafanyakazi karibu 300 kwa ajili ya kufanya kazi kwenye kampuni yao mpya.
Xiaomi hawasemi mengi kuhusu kampuni yao mpya iwapo watajikita katika kutengeneza magari yanayojiendesha yenyewe/yanayotumia nishati ya umeme ama kuwekeza kwenye kutoa suluhisho kote kwenye utengenezaji na upande wa programu wezeshi zinazofanya gari kufanya kazi.
Katika kampuni hiyo mpya Xiaomi wanatazamiwa kuwekeza $1.5 bilioni nyingine katika miaka inayokuja. Halikadhalika, haijafahamika ni lini tutaweza kuona gari ya kwanza inayotumia nishati ya umeme/inayoendeshwa bila dereva ya kwao Xiaomi.
Kumbuka kutufuatilia kupitia mitandao yetu ya kijamii ili kuweza kufahamu masuala mbalimbali yanayohusu teknolojia ndani na nje ya Tanzania tukikuhabarisha kwa lugha adhimu ya Kiswahili.
Vyanzo: GSMArena, Gizmochina, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.