fbpx

Ufaransa Kukataza Magari Ya ‘Petrol’ Na ‘Diesel’ Ifikapo 2040!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ufaransa ni nchi kubwa sana na inajiweza katika mambo mengi kama vile kiuchumi. Ukiachana na kuwa taifa kubwa kuna mambo mengi ambayo raisi mpya wa nchi hiyo anataka kuyaboresha.

Baada ya mambo hayo ni ikiwemo na hili la kutaka mpaka kufikia mwaka 2040 kusiwe na magari yoyote ambayo yanatumia nishati ya petrol au diesel nchini ufaransa.

Raisi Wa Ufaransa, Emmanuel Macron. Teknolojia Hii Ni Moja Kati Ya Mipango Yake Kama Raisi

Na hili limetokea baada ya siku chache tuu kampuni ya Volvo kusema kuanzia mwaka 2019 itaanza kutoa magari yanayotuumia nishati ya umeme

Soma zaidi Hapa.

Hili ni jambo zuri na linakuja kama njia moja ya kupunguza uharibifu wa mazingira (Hewa). Ni wazi kwamba mashine nyingi na ikiwemo magari huwa yanatoa hewa chafu ya ‘cabon’ ambayo inaharibu mazingira na inaathiri kwa kiasi kikubwa afya ya mwanadamu.

Moja Kati Ya Gari Ambalo Liinatumia Nishati Ya Umeme

Kufikia lengo hili pia kwa watengenezaji wa magari wa ufaransa sio jambo la mchezo mchezo kwani makampuni hayo inabidi yaje na magari ambayo hayatatumia nishati hizo kabisa.

Makampuni kama Renault na Peugeot-Citroen ni makampuni makubwa sana duniani lakini yapo katika presha kutokana na jambo hili.

Vile vile Raisi wa ufaransa amesema kuwa mpaka kufikia 2022 matumizi ya makaa ya mawe hayatatakiwa tena na hivyo basi teknolojia hiyo itahimia na kutumia umeme.

Ukiachana Na Sheli Za Mafuta Pengine Hii Inaweza Ikawa Alama Ya Eneo Ambalo Litatumika Kuchaji Magari Hayo Ya Nishati Ya Umeme

Kingine kizuri ni kwamba wamekadiria kwamba kama magari yanayotumia nishati ya mafuta (petrol na diesel) yanakaa baeabarani kwa muda wa miaka kumi na tano. Hii ni sawa na kusema kuwa mpaka 2055 ufaransa kutakuwa hakuna magari ambayo yanatumia nishati hizo kabisa.

Ningependa kusikia kutoka kwako kwa hili unaipa ufaransa asilimia ngapi? niandikie hapo chini sehemu ya comment.

kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com