fbpx

Hatimaye bajaji yenye kutumia nishati ya Jua yawasili Uingereza

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

‘Kwenye nia siku zote pana njia’. Usemi huu unadhihirika baada ya ile bajaj yenye kutumia nishati ya Jua kuwasili nchini Uingereza baada ya kukwama nchini Ufarasa kwa zaidi ya wiki moja.

Takribani wiki moja hivi TeknoKona ilikuhabarisha kuhusiana na bajaji iliyokwama safari yake kutokana na dereva wa bajaji hiyo kuibiwa nyaraka yake ya kusafiria (passport), hatimaye dereva bajaji hiyo amefanikiwa kufika Uingereza.

Mmiliki wa bajaji yenye kutumia nishati ya Jua.

Mmiliki wa bajaji yenye kutumia nishati ya Jua.

Safari hiyo ilidumu kwa miezi saba na umbali ukiwa maili 6,200 (9,978 Km). Alitarajia kufika mapema lakini akakwama kwa muda Paris baada ya pasipoti na kipochi chake kuibiwa.

Mhandisi Bw Rabelli akiwasili Uingereza.

Mhandisi Bw Rabelli akiwasili Uingereza.

Mmiliki wa bajaj hiyo alisema kuwa watu hupenda bajaji yake na hujitokeza na kupiga selfie. Watu hushangaa sana anapowaambia kuwa bajaji yake haitumii mafuta.

Alianzia safari yake Bangalore nchini India kisha akaendea Iran. Alipitia Uturuki, Bulgaria, Serbia, Austria,Uswizi, Ujerumani na Ufaransa. Anapanga kuhitimisha safari yake katika kasri la Buckingham, London.

INAYOHUSIANA  Nusu ya ajira zote kuchukuliwa na kompyuta ndani ya miaka 15

Ni safari iliyokuwa na changamoto kadhaa lakini hatimaye lengo la  kuhamaisha watu kutumia magari yanayotumia kawi mbadala kama vile solar au umeme limetimia.

Vyanzo: BBC, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.