Mwaka 2018 umekuwa ni wenye mambo mengi yaliyoiletea Facebook misukosuko ambayo imeigharimu kampuni hiyo kiasi kikubwa kuanzia heshima yake mpaka kifedha lakini sasa imeamua kujihami kabla ya hatari.
Naamini utakuwa unakumbuka vyema sakata la Facebook na Cambridge Analytica kitu ambacho kimesababisha mpaka sasa bado mhusika mkuu analipa gharama ya makosa yake kwa namna tofauti tofauti.
Hivi karibuni Facebook wamesitisha ushirikiano na programu tumishi zaidi ya 400 kwa sababu ya hofu ya matumizi ya taarifa za watu isivyostahili au kuwa na mashaka kwa yule aliyetengeneza programu husika.
Wakati wa sakata la Facebook na Cambridge Analytica taarifa za watu takribani 87m zilitumiwa isivyopasa hivyo basi hivi sasa kampuni hiyo maarufu zaidi duniani inafanya juhudi zote wasijerudia kosa.
Vyanzo: The Citizen Tz, SABC News