fbpx
M-Pesa, Mitandao ya Simu, Tanzania, Teknolojia

Vodacom na TPB kusaidia wateja wanapopungukiwa na salio

vodacom-na-tpb-kusaidia-wateja
Sambaza

Katika ulimwengu wa sasa mtindo wa kutembea na pesa nyingi mfukoni si kitu kizuri kabisa na mbadala wake umekuwa makampuni ya mitandao ya simu halidhalika taasisi za fedha. Ndio, na hivi sasa wateja wa Vodacom Tanzania hasa M-Pesa wanafurahi sasa.

KIla sekunde inayopita basi kuna mahali muamala wa pesa unafanyikaikiwa kama njia rahisi ya kuhifadhi, kutuma/kupokea pesa ndani na nje ya Tanzania. Hii yote inatokana na ukuaji wa teknolojia iliyowezesha watu wengi kuweza kuwa na mwamo wa kutumia simu kwa ajili ya mawasiliano/miamala.

INAYOHUSIANA  IG kwa ajili ya kuuza au kununua bidhaa

Ni siku moja imepita baada ya Vodacom na TPB (Benki ya Posta Tanzania) kuingia makubaliano kibiashara ambapo wateja pande hizo mbili watanufaika; hakuna tena muamala kukwama kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha, kupitia huduma ya Songesha na M-Pesa” mteja ataweza kujinga na iwapo alikuwa anafanya anataka kulipia huduma basi ataongezewa kiasi kilichopungua.

Kiwango cha riba ya 1% atatozwa kwa siku moja iwapo atatumia huduma ya Songesha na M-Pesa; wingi/uchache wa kuomba msaada utatokana na alama unakazopata kutokana na miamala unayofanya na hapo ndipo benki ya Posta Tanzania inapoingia kutokana na kutumia mifumo yao kujua ukomo wa kuomba msaada kwenye M-Pesa kulingana na unavyotumia huduma (M-Pesa).

Vodacom na TPB
Vodacom na TPB wawaangalia wateja wa M-Pesa kwa jicho la karibu hatimae kuleta huduma mpya.

Huduma hiyo mpya itawawezeha wateja wa M-Pesa kutopata wakati mgumu wakati wa kulipia huduma mbalimbali. Ni matumaini yangu picha jongefu hapo chini itakusaidia kuelewa zaidi.

Vyanzo: Vodacom Tanzania, EATV

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|