fbpx

Huawei kutoa mafunzo kwa wahitimu wa vyuo

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

vodacom swahili

Sambaza

Wahitimu kutoka vyuo mbalimbali wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kuwa uwezo wa kuitumia vyema ile elimu aliyoipta katika chuo kikuu jambo ambalo ni tatizo kubwa kwa wahitimu wa vyuo mbalimbali Tanzania.

Tumekuwa tukitumia bidhaa za Hiawei kwa miaka kadhaa sasa na ni wazi kwamba vinavyotengenzwa na kampuni hiyo vimepata soko kubwa tu barani Afrika na duniani kwa ujumla sasa ni zamu ya upande wa pili wa shilingi, Agosti 20 2018 ilizindua programu ya kutoa mafunzo kwa wahitimu wa vyuo ikilenga wahitimu kutoka UDOM na UDSM.

Programu hiyo ya mafunzo itakuwa inahusu masuala ya TEHAMA itakayoendeshwa na wataalam waliobobea kutoka Huawei Co. Technologies lengo likiwa ni kuondoa uwazi uliopo kati ya nadharia na mafunzo ya vitendo lakini pia kuwa na uwelewa mpana zaidi kuhusu sekta ya habari na mawasiliano ulimwenguni.

Programu ya Tanzania Seeds For the Future ilianza miaka mitatu iliyopita huku kila mwaka wahitimu 10 wanachaguliwa kwenda makao makuu ya Huawei, Shenzhen-Beijing kujifunza mengi na kujionea teknolojia za kisasa zinazozitumia Huawei.

wahitimu wa vyuo

Afisa Mkuu wa Huawei kwa Tanzania, Bw. Gao Mengdong akizungumza wakati wa uzinduzi programu ya mafunzo ya TEHAMA kwa wahitimu wavyuoni.

Mafunzo kama hayo yamekuwa yakitolewa kwa miaka kadhaa kwa nchi mbalimbali Afika kama vile Afrika Kusunu, Kenya, Ghana, Botswana na Angola huku Huawei wakitoa mafunzo hayo katika vyuo vingi zaidi nchini A. Kusini kuzidi nchi nyingine ambapo programu huyo inaendeshwa.

INAYOHUSIANA  Huawei yashikwa kwa picha Feki, ujio wa simu yake mpya ya P30 PRO

Programu hiyo pia inatoa nafasi kwa wanahitimu kutoka Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) pamoja na Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA).

Chanzo: IPP Media

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.