fbpx
Android, apps, Google

Programu tumishi ya Play Music kusitishwa mwezi Desemba

programu-tumishi-ya-play-music-kusitishwa-mwezi-desemba

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Wale wote wanaotunia Play Music kusikiliza nyimbo mbalimbali basi wafamu ya kuwa wana miezi nne tu ya kuendelea kutumia programu tumishi husika.

Imekuwa ni taarifa ya ghafla kutokana na Google kutangaza itasitisha matumizi ya programu tumishi iitwayo Play Music ifikapo mwezi Desemba mwaka huu. Habari hizi zilikuwepo kwa muda tuu ingawa haikuwa imefahamika ni lini mpango huo utatekelezwa.

INAYOHUSIANA  WhatsApp yaanzisha huduma ya kutumiana Pesa

Katika siku za usoni Google watasitisha uwezo wa kupakia/kupakua nyimbo kutoka kwenye programu tumishi husika lakini pia kutopatikana kwenye programu wezeshi mahususi kwa saa janja zinazotumia mfumo wa Android (Wear OS).

Kinachotakiwa kufanynika hivi sasa.

Google inashauri wale wote wenye vitu vyao kwenye Play Music wavihamishe kwenda YouTube Music kwa kutumia Google takeout au “Kifaa cha kuhamisha“. Mwezi Septemba, huduma ya kusikiliza muziki bila kuupakua itasitishwa kwenye nchi za Afrika Kusini na New Zealand halafu Oktoba 2020 itakuwa duniani kote.

INAYOHUSIANA  Facebook Pages: Kuonekana/kutoonekana kwa ukurasa
Play Music
Google yaamua kuipa nguvu YouTube Music kwa kuachana moja ya programu tumishi inayozimiliki.

Vilevile, mwezi Oktoba Google wataondoa hewani tovuti ya programu tumishi husika lakini pia kuiondoa kwenye Google Playstore ingawa watatunza data za watu mpaka mwezi Desemba kwa wao kuweza kuhamisha viytu hivyo na kwa ambao watakuwa hajafanya hivyo mara baada ya muda uliowekwa kupita watapoteza huduma zote ambazo walilipia ndani ya Google Play Music.

Haya sasa ewe msomaji wetu sisi tumeshakuhabarisha, fanya hima uweze kuhamishia vitu vyako kwenye YouTube kwani “Wakati ni ukuta!”.

Vyanzo: TechCrunch, TechSpot

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|