Katika mahojiano na mtandao wa Bloomberg, mkurugenzi mtendaji wa Apple bwana Tim Cook amethibitisha tetesi ambazo zimekuwako kwa muda mrefu sasa juu ya kampuni hiyo kutengeneza gari .
Kuthibitishwa kwa uwepo wa kampuni hiyo katika kinyang’anyiro hiki cha utengenezaji wa magari bora kunaongeza chachu na ushindani kwa watengenezaji wengine wa magari.
Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba mradi wa magari wa Apple ni majumuisho ya Teknolojia ya magari ya kujiendesha yenyewe,magari yanayoendeshwa kwa nguvu za umeme na pia mpango wa magari ya kijamaa (kama Uber)

Taarifa hii imeamsha tetesi ambazo zimekuwapo kwa muda mrefu kwamba kampuni hii yenye thamani zaidi duniani inafanyia kazi mradi wa magari. Mahojiano haya yameweka wazi kwamba Apple wanafikiria kujihusisha zaidi katika kutengeneza mfumo utakao tumiwa na magari, yaani sio lazima wakatengeneza magari kabisa ila wanataka kutengeneza mfumo utakao tumiwa na magari.