fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Nokia Teknolojia

Android 11 yafikishwa kwenye simu janja Nokia 5.4

Android 11 yafikishwa kwenye simu janja Nokia 5.4

Spread the love

Mapema mwezi Mei mwaka huu Nokia ilitoa orodha ya simu zake ambazo zitapokea masasisho hivyo kuwea kuhamia Android 11 na miongoni mwa rununu hizo ni Nokia 5.4.

Wakati watu wengi wakisubiri ujio rasmi wa Android 12 kuna simu nyingi kadha wa kadha bado hazijaweza kuhamia kwenye toleo la sasa la programu endeshi la sasa; Nokia 5.4 imeingia kwenye orodha ya simu janja ambazo zimeshaanza kupokea taarifa fupi ya kuweza kupakua masasisho na kuhamia Android 11.

SOMA PIA  Nichague Mtandao Upi Kwa Ajili ya Matumizi ya Intaneti?

Nokia 5.3 yenyewe ilipokea taarifa ya kuweza kuhamia kwenye toleo hilo la sasa la programu endeshi mwezi Agosti mwaka huu, Nokia 3.4 ikapata wiki chache baadae. Nokia 2.4 ikafikiwa mapema mwezi Aprili. Watumiaji wa Nokia 5.4 kwenye nchi mbalimbali wameanza kupelekewa taarifa fupi ya kuweza kuhamia Android 11 mwezi huu.

Sasisho linakuja pamoja na maboresho mengine ya usalama wa simu janja kati ya mwezi Juni-Agosti pamoja na vitu vingine ambavyo vimeboreshwa kwa lengo la kuzidisha ufanisi wa rununu husika.

simu janja Nokia

Android 11 yafika kwenye simu janja Nokia 5.4.

Toleo hilo la programu endeshi lina ukubwa GB 1.77 na kuna vitu vizuri ambavyo vinapatikana kwenye Android 11 kama ambavyo wanaotumia toleo hilo wanaweza kuthibitisha.

SOMA PIA  Instagram Wabadili Maamuzi!

TeknoKona ushauri wetu ni daima tukumbuke kuhakikisha kuwa simu inakuwa na chaji zaidi ya 50%, kifurushi cha intaneti ambacho kinazidi GB 1.8 bila kusahau uwepo wa nafasi kwenye memori angalau GB 1.8 na zaidi.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania