Watu wengi wenye simu janja kutumia WhatsApp ni kitu cha kawaida sana katika hali ya kuweza kuwasiliana na mtu kwa haraka na wepesi lakini pia maboresho mapya yanatoka kila mara na sasa wametanua wigo kuhusu uwezo wa kutafuta kitu.
Mara nyingi mtu akiniuliza ni WhatsApp gani bora (kwa zilizo rasmi) kutumia? Jibu langu huwa ni rahisi tuu kwamba toleo la Beta linafaa zaidi. Sababu ya jibu hilo ni kwamba watumiaji wa WhasApp Beta wanakuwa watu wa kwanza kabisa kupata maboresho yaliyo katika hatua ya majaribio kabla ya kupatikana kwa wengine wote.
Sasa kwenye WhatsApp Beta kati ya toleo namba 2.20.197.7 na 2.20.197.10 wamepata kuona jinsi gani kipengele cha kutafuta kitu kilivyoongezewa makali. Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, WABetaInfo wameonyesha kipengele cha kutafuta mtu anaweza akapekua picha, nyaraka, picha mnato, n.k ndani ya WhatsApp Beta.

Huu ni muendelezo tuu wa mapya kuongezwa kwenye WhatsApp kama ambavyo siku kadhaa zilizopita tulivyowaletea makala kuhusu ni kwa muda gani mtumiaji anaweza akaamua jumbe ziingie kimya kimya.
Wewe msomaji wetu una maoni gani kuhusu uwezo wa kutafuta kitu kwa mapana zaidi ndani ya WhatsApp Beta? Tupe maoni yako na daima usiache kutufuatilia kwa habari kedekede zinazohusu ulimwengu wa teknolojia.
VyanzO: Gadgets 360, WABetaInfo