fbpx

Google, Google Drive, Teknolojia

Google Drive: Mafaili kwenye kapu la uchafu kufutwa baada ya siku 30

google-drive-mafaili-kwenye-kapu-la-uchafu-kufutwa-baada-ya-siku-30

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Ikiwa huna mazoea ya kufuatilia kopo la uchafu kwenye Google Drive basi hakikisha unafanya kama tabia kufuatilia kuanzia sasa.  Google imetangaza kuwa itafuta faili zote zilizowekwa kwenye kapu la takataka baada ya siku 30.

Hapo awali, Trash folder zilihifadhiwa milele isipokuwa ukienda kwenye kapu la uchafu na ukaifuta kabisa.  Hii iliruhusu watumiaji kupata faili kwa urahisi pale anapolihitaji.

Sera hii itaanza kutumika kuanzia Oktoba 13 na mara tu itakapoanza kutumika kutakuwepo taarifa fupi kwenye Google Drive, Hati za Google na Fomu za Google kueleza kuhusu mabadiliko hayo kuanzia Septemba 29. Mabadiliko ya sera yataanza kutekelezwa bila kujali anakubali/kukataa mabadiliko hayo.

Tufahamu ya kuwa kuweka vitu kwenye kapu la takaktaka ndani ya Google Drive kisha kuvifuta kabisa si kwamba vinatoweka kabisa la hasha! Waangalizi wanao uwezo wa kuvirudisha vitu vilivyofutwa ndani ya siku 25 kwa wale watumiaji hai.

Google Drive
Kwenye Google Drive vitu vinahifadhiwa sehemu ambayo kwa lugha ya kawaida tunaweza kusema “Pasipojulikana/hewani” kutokana na uwezo wa kuviapta muda wowote ambao mtumiaji atahitaji.

Sera za utunzaji zilizowekwa na wasimamizi katika Google Vault haziathiriwi na mabadiliko haya, isipokuwa yatakapopitwa na wakati kwani sasa hayatumiki. 

Mabadiliko haya huathiri vitu ambavyo vimetupwa kutoka kwa kifaa chochote na jukwaa lolote maadamu viko kwenye akaunti sawa ya Google. Je, unadhani mabadiliko haya yatamuathiri mtumiaji kwa kiasi gani?

Vyanzo: The Verge, Times of India

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Richard Kiwanga

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*