fbpx
instagram, Teknolojia

Umesikia kuhusu Reels ndani ya Instagram?

umesikia-kuhusu-reels-ndani-ya-instagram
Sambaza

Katika ulimwengu wa “Kileo” watu wengi duniani wana akaunti Instagram ambayo imekuwa kivutio cha cha watu duniani kote na hata kusababisha uraibu. Sasa wamezindua “Reels“.

Uweo wa kupakia picha jongefu ambazo si ndefu (kati ya sekunde 15 hadi 60) zimekuwa kivutio cha wengi ambapo hivi sasa TikTok ipo katika umaarufu wake na hata kupatikana katika nchi takribani 50 duniani kote. Instagram nao wakaona kuna haja ya kuleta mpinzani waliyemuita “Reels“.

INAYOHUSIANA  Vitu vipya kwenye WhatsApp safari hii

Kipengele hiki kipya kinapatikana ndani ya Instagram kwenye kitufe cha kamera kilichopo upande wa kushoto juu ambapo mtumiaji anaweza akarekodi picha mnato ya urefu wa sekunde 15, kuweza kuiwekea ujumbe wa sauti pamoja na nakshi nakshi nyningine nyingi tuu kisha kuipeleka hewani kwa watu kuweza kuitazama.

Reels
Instagram waleta “Reels” kupambana na TIkTok.

Upo uwezekano pia wa kuitunza kwa muda fulani kwa lengo la kutaka kufanyia maboresho kadha wa kadha kabla ya kuiruhusu kwenda hewani, kuweza kubadilisha picha ya ukurasa (cover photo). Machapisho yote ya “Reels” yanaonekana kwenye kipengele cha “Feed” au “Discover tab“.

INAYOHUSIANA  WhatsApp, Facebook na Instagram zapata shida: Fahamu maeneo yaliyoathirika
Reels
Sasa unaweza ukaamua kutumia Reels ama TIkTok.

Unajiuliza kama kimeshawafikia watumiaji wa Instagram bara la Afrika? Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali nchi ambazo kipengele hicho kimeshafika ni Marekani, Uingereza, Ufaransa, Japan, Brazil, Australia, Ujerumani na India.

Vyanzo: The Verge, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|