fbpx

apps, whatsapp

WhatsApp yaanzisha huduma ya kutumiana Pesa

whatsapp-yaanzisha-huduma-ya-kutumiana-pesa

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Baada ya miezi ya kadhaa ya tetesi hatimaye wamiliki wa app ya WhatsApp wamezindua huduma ya malipo ya kutuma pesa kutoka kwa mtumiaji mmoja mpaka mwingine kwa nchi ya Brazil.

Huduma hiyo imeanza rasmi masaa machache yaliyopita kwa nchi hiyo yenye watumia wa WhatsApp takribani
milioni 120. Huduma hiyo itakuwa inapatikana bila ya kumuathiri mtumiaji kwenye matumizi yake ya mengine ya mawasiliano.

Mfumo huo wa utumaji pesa umeunganishwa na ule wa Facebook pay ulioanza mwaka mmoja uliopita. Aidha kwa watumiaji wa iOS wataunganishwa na Messages app.

WhatsApp yaanzisha huduma ya kutumiana Pesa
WhatsApp yaanzisha huduma ya kutumiana Pesa

 

Ili mtumiaji aweze kutuma au kupokea pesa atalazimika kuunganisha akaunti yake ya
WhatsApp na kadi yake ya Benki aidha ya Visa Card, Mastercard au Debit card.

Hata hivyo huduma hii kuanza nchini Brazil imewashangaza wengi badala ya nchi ya India ambayo kwa miezi kadhaa WhatsApp imekuwa kwenye majaribio ya huduma ya malipo kupitia Unified Payments Interface(UPI).

INAYOHUSIANA  Facebook Waja na Hello : App Mpya kwa Simu za Android

Aidha huduma hii itawafurahisha wengi kwa kuwa watumiaji wa WhatsApp wamekuwa wakifanya biashara ya bidhaa kadhaa kupitia Programu hiyo na kulazimika kutumia njia zingine za malipo.  Lakini sasa yote yatamalizwa kupitia hapo hapo WhatsApp.

WhatsApp tangu kununuliwa na Facebook mwaka 2014 imeendelea kuboresha huduma zake kila kukicha. Mbali na kutoa fursa za watumiaji wake kuweza kuandikiana ujumbe, kupigiana simu za sauti na Video, sasa
inawapa nafasi nyingine watumiaji wake kuweza kutumiana pesa.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.