fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android apps Intaneti Kompyuta Maujanja simu Teknolojia Uchambuzi USSD

Fahamu kuhusu USSD CODE na Maujanja yake.

Fahamu kuhusu USSD CODE na Maujanja yake.

Spread the love

USSD Code ni itifaki ya mawasiliano inayotumiwa na simu za mkononi kuwasiliana na kompyuta za waendeshaji wa mtandao wa simu. USSD inaweza kutumika kwenye kivinjari kwa WAP, huduma za kulipia, huduma za pesa, huduma za maudhui kulingana na eneo, huduma za habari zinazotegemea menyu, na kama sehemu ya kusajili simu kwenye mtandao.

Katika matumizi yetu ya kawaida tumekuwa tukitumia sana hizi USSD Code kupitia mitandao mbalimbali ya simu kama Tigo, Vodacom, Airtel na Halotel. Leo teknokona tumekuandalia orodha ya USSD Code zitakazokuongezea maujanja ambazo ni:

SOMA PIA  Uganda: Sheria ya kodi ya mitandao ya kijamii kupitiwa upya

Kupima hali ya simu: Unaweza kupima hali ya simu kwa kujaza tarakimu zifuatazo (*#0*#), ambapo utaonyeshwa menyu ya kuchagua ni uwezo upi wa simu janja yako unaotaka kuupima.

Kuangalia IMEI namba ya simu: Endapo utahitaji kujua IMEI namba ya simu janja yako unaweza kuiangalia kwa kubofya tarakimu zifuatazo kwenye simu janja yako (*#06#). Baada ya kuona IMEI namba yako unaweza kuirekodi pembeni kwaajili ya matumizi ya baadae.

SOMA PIA  Space X ya rusha na kisha kuirudisha roketi duniani salama (kwa mara nyingine).

Kuangalia kama simu yako inasikilizwa: Unapokuwa na mashaka yoyote kuhusu simu yako kusikilizwa au ujumbe kusomwa na mtu mwingine unaweza kutumia tarakimu hizi kuchunguza hali hii (*#67#). Kupitia njia hii utaweza kuona kama maongezi yako yanasikilizwa au jumbe zako zinasomwa. Pia ukitaka kuona ni namba gani ya simu inasikiliza au kusoma jumbe zako utatumia tarakimu (*#61#).

USSD CODE

Kuficha uwepo wako kwenye programu za Caller ID: Kujali faragha yako ni jambo la msingi hivyo kutokana na watu wengi kutumia programu za Caller ID siku hizi unawea kutumia tarakimu zifuatazo (#31#) kuzuia mtu kukutambua kupitia programu hizo.  Kwa orodha ya USSD Code zingine tembelea tovuti hii.

SOMA PIA  Walmart: Sasa Kuagiza Vyakula Kutumia Kifaa cha Sauti cha Google

USSD CODE

Tupe maoni yako kuhusu makala hii na pia tueleze kama taarifa hizi zimekusaidia kwa namna moja ama nyingine katika matumizi yako ya simu janja. Endelea kutembelea tovuti yetu kujifunza zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake na pia kupata habari mbalimbali za kiteknolojia. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania