fbpx
Android, apps, Teknolojia, whatsapp

Ukimya kwenye WhatsApp waendelea kuboreshwa

ukimya-kwenye-whatsapp-waendelea-kuboreshwa
Sambaza

Katika ulimwengu mawasiliano kupitia vifaa vya kiganjani unapamba moto siku hadi siku kitu ambacho wengi wetu tumekuwa tukitumia WhatsApp kwa kiasi kikubwa tuu; pengine hata kuishia kuweka kifurushi cha intaneti pekee.

Tangu kuanza kutumia kwa WhatsApp Mei 3 2009 hadi leo hii maboresho mengi sana ambayo yamewekwa kwenye programu tumishi husika na kufanya ivutie zaidi lakini tukizungumzia suala zima la faragha ndio linazidi kuwa murua kweli.

INAYOHUSIANA  eWater: Mfumo wa kupata maji safi muda wowote kwa njia ya kidigitali

Unaweza ukawa ni mmojawapo kati ya watu wengi wanaopenda “Ukimya kwenye WhatsApp” kwa maana ya kwamba jumbe nyingi tuu umeziamuru kuweza kuzifikia bila ya wewe kupata taarifa au kujulishwa ingawa bila sauti kutoka.

Sasa ni vyema ukafahamu kuwa kulingana na toleo la 2.20.197.3 kwenye WhatsApp Beta mtumiaji anaweza akaamuru daima asiweze kusikia sauti ya ujumbe unapoingia kutoka kwa mtu ama kundi/vikundi.

Ukimya kwenye WhatsApp
Kwenye WhatsApp Beta mtumiaji anaweza akachagua kutosikia sauti ya ujumbe unapoingia siku zote (daima).

VIlevile, WhatsApp wanaonekana kurudisha machoni pa watu kipengele cha jumbe kuweza kufutika baada ya muda fulani kupita (siku 7) na hii ni kwa mujibu wa WABetaInfo ikionyesha mtu anaweza kukiruhusu au kutokukiruhusu kufanya kazi yake.

INAYOHUSIANA  Google watambulisha simu mpya, zifahamu Google Pixel na Pixel XL
Ukimya kwenye WhatsApp
WhatsApp Beta toleo la 2.20.197.4 linamuwezesha mtumiaji kuweza kuwasha/kuzima kipengele ambacho kinaruhusu ujumbe/jumbe kufutika baada ya siku saba kupita.

Hiyo ndio WhatsApp Beta na ukimya kwenye WhatsApp ambapo watumiaji wake wanapata kupokea masasisho kabla ya wengine wote. Vipi wewe msomaji wetu una neno la kusema kuhusu maboresho hayo?

Vyanzo: Gadgets 360, WABetaInfo

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. WhatsApp watanua wigo kuhusu uwezo wa kutafuta kitu
    August 6, 2020 at 11:52 pm

    […] Huu ni muendelezo tuu wa mapya kuongezwa kwenye WhatsApp kama ambavyo siku kadhaa zilizopita tulivyowaletea makala kuhusu ni kwa muda gani mtumiaji anaweza akaamua jumbe ziingie kimya kimya. […]