fbpx

WhatsApp na machapisho ya picha za mnato

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Unapotaka kitu kivutie basi jambo ambalo unaweza kufikiria ni kuboresha kila mara unapoona kuwa kuna umuhimu wa kufanya hivyo vivyo hivyo WhatsApp na machapisho ya picha mnato kutoka Facebook na Instagram.

Katika makala zangu kadha wa kadha zinazohusu masasisho kwenye WhatsApp huwa nashauri sana watu waweze kutumia toleo la WhatsApp BETA na hii ni kwa sababu kuu moja tu; masasisho yote yanayohusu programu hiyo huwa yanaanzia huko kabla ya kuruhusiwa kwa wengine.

Kwa wanaotumia toleo ambalo ni la majaribio kwenye WhatsApp (Beta v2.18.301) wanaweza kucheza picha jongefu zilizotoka kwenye machapisho ya Facebook au Instagram bila kupelekwa sehemu ambapo picha mnato imechapishwa.

WhatsApp na machapisho

WhatsApp BETA inayowezesha kucheza picha mnato zilizotoka Facebook/Instagram bila ya kwenda kwenye mtandao husika kuweza kuzitazama.

Kwa wanaotumia iOS ambacho kimefika kwenye Android sio jambo geni kwao kwani ilianzia huko kabla ya kuletwa upande wa pili.

Masasisho hayo bado hajaanza kupatikana kwa watumiaji wote wa WhatsApp kwenye Android na hata picha mnato kutoka Twitter zitafunguka kwenye uwanja tofauti (sio kama za kutoka kwenye Facebook au Instagram).

Vyanzo: GSMArena, Android Police

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Kuhusu Google Pixel 3a na 3a XL sio fununu tena
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.