fbpx

Huawei: Waadhibiwa kwa kosa la kuchapisha habari kwa kutumia iPhone

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Unaweza ukawa na simu janja ya kampuni fulani lakini sasa hauruhusiwi kuitumia kwa ajili ya kazi fulani vinginevyo utajikuta matatizoni na kuishia kuadhibiwa kutokana na kosa fulani.

Teknolojia haifichi kitu labda uwe mjanja mjanja kwa kutumia njia za kujificha lakini mwisho wa yote unapata matokeo ambayo ulikuwa unayategemea. Huawei imeamua kuwaadhibu wafanyakazi wanaangalia kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii kwa kosa la kuchapisha taarifa za kwao kwenye Twitter kwa kutumia iPhone.

Ilikuaje?

Wengi wentu tunafahamu sio jambo rahisi kutumia mitandao ya kijamii nchini Uchina sasa programu ya VPN kwenye kompyuta ilileta shida kwahiyo ikawa tabu kuingia Twitter. Lakini ilikuwepo iPhone ambayo ilikuwa imewekwa kadi ya nchi nyingine basi ndio mtu anayesimamia ukurasa wa Twitter wa kampuni ya Huawei Technologies akaitumia kuchapisha ujumbe wa heri ya mwaka mpya.

Kitendo hicho kimeleta shida kwenye bodi ya Huawei Technologies wameadhibiwa kwa kukwatwa mshahara wa karibu $278 kila mwezi lakini kushushwa cheo kwa mmoja wa wafanyakazi hao huku mshahara ambao anastahili kulipwa ukiwekwa kando kwa kipindi cha mwaka mmoja.

kuchapisha

Chapisho la Huawei kwenye Twitter lililowafanya wafanyakazi wawili waaddhibiwe.

Hapo ndio huwa napenda kusema “Ajali kazini” lakini mwisho wa siku ni lazima uonje shubiri ya makosa yako.

Vyanzo: The Verge, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  App ya kujitegemea ya Instagram Direct kuondolewa!
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.