fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Teknolojia

Ni ruksa kutoa talaka kwa njia ya simu nchini Saudia

Ni ruksa kutoa talaka kwa njia ya simu nchini Saudia

Spread the love

Simu zetu zinatumika katika kufanikisha mambo mbalimbali katika dunia ya leo na kwa wengine inaweza ikaonekana ni dharau lakini nchini Saudia mahakama imeridhia talaka kwa njia ya simu.

Wakati fulani nilishawahi kuandika kuhusu marufuku kutoa TALAKA kwa njia ya simu huko Tanzania Zanzibar lakini kwa nchi kama Saudia  Arabia imeonekana kuwa itasaidia kuwaokoa watalakiwa.

SOMA PIA  Marufuku matumizi ya Bitcoin nchini Iran

Kwanini utoaji wa talaka umeruhusiwa nchini Saudia?

Nchini humo (Saudia Arabia) kabla ya sheria ya utoji talaka kwa njia ya simu (ujumbe mfupi wa maandishi) kupewa baraka na mahakama iliwezekana kupewa talaka ya siri jambo ambalo lilimfanya mwanamke kutojua kama ameshatalakiwa na hivyo kushindwa kudai haki zake.

nchini Saudia

Wanawake wa Saudia Arabia kupewa taarifa kuhusu kupewa talaka kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno.

Kujua kuwa mwanamke amepewa talaka kwa njia ya simu itasaidia?

Kwa mujibu wa wanawake, wanasheria wanawake waliokuwa wanapigania sheria hiyo ipite wamesema kuwa njia hiyo ya kumtaarifu mwanamke kuwa ametalakiwa itamsaidia kuwa na ushahidi ambao utamuweka katika nafasi ya kuweza kudai haki yake kwa muda wote alioishi na huyo mwanaume.

SOMA PIA  Kasi ya intaneti inaongezeka duniani kote! #Ripoti #Akamai

Sheria hiyo ilipata msukumo mkubwa wa kupitishwa/kukubaliwa baada ya kuwepo malalamiko mengi yaliyopo mahakamani kuhusu mwanamke kupewa talaka bila kujua.

Vyanzo: The Times of ISrael, Khaleed Times

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania