Imekuwa ni mojawapo ya njia rahisi kuwashirikisha wengine iwe ni katika mfumo wa maandishi, picha au hata picha jongefu kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine/wengine lakini sasa kusambaza kitu kumeweka ukomo!
Sote tunafahamu kuwa kwenye WhatsApp inawezekana kumtumia mtu kitu kwa njia ya kunakili kisha ukakituma kwa mtu/watu mara nyingi tuu lakini WhatsApp amabayo ipo chini ya Facebook wameamua kuruhusu ujmbe au kitu kiweze kusambazwa sio zaidi ya mara tano (5).
Nini sababu ya kupunguza uwezo wa kusambaza kitu kwenye WhatsApp?
Kwa mara ya kwanza kipengele hicho kilitambulisha kwa watumiaji wa WhatsApp nchini India ikiwa kama njia ya kukabiliana na usambazaji wa taarifa za uwongo kwa watu. Nchi kama Brazil walipata shida sana kuhusu suala la taarifa zisizo za ukweli lakini hata nchini Marekani wana shida hiyo.
Tafsiri yake ni nini?
Ingawa WhatsApp wamepunguza ule uwezo wa mtu kuweza kuwasambazia watu taarifa mpaka mara tano pekee lakini fahamu hii:
unaweza ukatuma kwa watu watano pekee lakini kama ukituma ujumbe husika kwenye kundi/makundi ambalo linaweza kuwa na washiriki 256 kwa idadi basi ujumbe huo utakwenda kwa watu wapatao 1,300.
Ujumbe uliosambazwa kwenye WhatsApp: Mpaka kufikia mwezi Julai 2018 iliwezekana kutuma kimoja mara 20.
Ingawa WhatsApp wameleta mbadiliko lakini mtu anaweza akanakili kisha akaweka kwenye sehemu ya kuandika ujumbe kwenda kwa mtu kisha akautuma jambo ambalo hautakuwa na kichwa habari “Forwarded” hivyo basi mtu atakuwa ana uwezo wa kutuma ujumbe mmoja zaidi ya mara tano 😆 😆 😆 .
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|