Kama moja yakiashiria cha ukuaji wa teknolojia mitandao ya kijamii imekuwa ikitumiwa kwa njia mbalimbali kitu ambacho kinasababisha uwepo wa habari mbalimbali, sasa katika taarifa ya hivi karibuni Instagram wanapambana kuondoa vitu vya uwongo.
Mtandao wa kijamii umekuwa ukilaumiwa kutokana na kuwa sehemu ambayo taarifa zisizokuwa za kweli kuchapishwa na hivyo kusababisha upotoshaji, malumbano, n.k lakini hata hivyo wahusika wamekuwa wakijitahidi kuondoa mambo mbalimbali ambayo si ya kweli.
Katika maboresho ya hivi karibuni kupitia taarifa rasmi Instagram inatumia mbinu mpya ambayo inaweza kutambua akaunti ya uwongo, watu wasio wa kweli wanaofuta akaunti, maoni ya uwongo, n.k zilizotokana na kutumia programu tumishi ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kutuma maoni/kuongeza watu wanaokufuata kwa manufaa ya mwenye akaunti.
Katika kukabiliana na hilo wahusika wanatoa onyo na kuamjulisha mhusika kubadili nenosiri la akaunti yake kwa yeyote yule ambae alitumia programu za aina hiyo kujiongezea watu/kutuma maoni mabaya.
Sasa wale ambao walikuwa wakitumia njia zisizoeleweka kuongeza watu mnabidi mjihadhari kweli kweli.
Vyanzo: Tech Crunch, GSMArena