Mwaka Mmoja umepita tangu Vaio (Visual Audio Intelligent Organizer) wapewe uhuru na kampuni ya Sony, Kampuni hiyo (vaio) ina mpango wa kuachia simu yake ya kwanza kabisa. Kabla ya vaio kununuliwa na ‘Japan Industrial Partners’ kampuni hiyo ilikua ikimilikiwa na kampuni mama yaani Sony.
Vaio kwa ujio wao wa kwanza kabisa katika simu, wamekuja na simu janja yenye Os ya Android. Bei ya simu hiyo imekadiriwa kuwa kati ya dola za kimarekani 420.
Japokua simu hii ina tegemewa kuuzwa Japan tuu tena haswa kwa toleo hili. Ndani ya simu hii ya Vaio kuna prosesa ya ‘1.2 GHz quad-core ‘ ambayo inajumuisha ram ya GB2 na GB 16 za memori kadi ya nje ambayo inaweza kuongezeka mpaka GB 64.
Simu ina Kioo cha inchi 5 na kioo hicho ni cha 1280 x 720 HD (high definition), Kamera ya nyuma ina MP (Mega Pixels) 13, Na kamera yake ya Selfie (kamera ya mbele) ina MP 5.
Simu hii ya Vaio ambayo itapatikana kwa rangi nyeusi ni nyembamba kwa kiwango cha 7.95 mm na ina ujazo wa gramu 130, betri yake ni ya 2,500 mAh.
Wateja wengi bado wanazani Vaio wanaingiliana kwa namna flani na laptop za Sony. Vaio (Visual Audio Intelligent Organizer) imeuzwa na Sony kwa kampuni nyingine ya Japan mwaka 2014 na hii ni baada ya kuuza biashara yake ya kompyuta kwa kampuni hiyo (Japan Industrial Partners).
Wakati wawekezaji wengi na wachambuzi wengi wametoa mawazo yao kuwa sony wangeweza, wantakiwa waachane au wajitoe katika soko la simu ambalo linajumuisha simu janja na tablet, kampuni hilo (sony) ndio kwanza limefumba masikio na hivi karibuni wametangaza bidhaa zao mpya.
Simu mpya ya Vaio inaonyesha hadharani kuwa kutakua na ushindani kati ya simu hiyo na zile za Sony za matoleo ya Xperia na watafanya hivyo katika uwanja wa nyumbani Japan. Inategemewa mafanikio ya toleo hili yanaweza kuwafanya kuingia katika soko la dunia kabisa.
No Comment! Be the first one.