Tigo imetangaza kuwabadilishia wateja wake wote ambao wanatumia simu feki na kuwapatia simu orijino ili waendelee kupata huduma za simu hata pindi ambapo simu hizo zitakapokuwa zimezimwa na TCRA.
Mwanzoni mwaka huu TCRA ilitangaza kuzima simu zote ambazo sio orijino ifikapo tarehe 16/06/2016 na toka tangazo hili kutoka kumekuwa na sintofahamu kwa watumiaji wa simu Tanzania ambao mpaka mwaka 2015 walikuwa wanafikia takribani milioni 34.108.
sharti = kujiunga na kifurushi spesheli cha dakika 350 sms 1000 na mb 250 ambacho ni shilingi 22000/=
David Zachariah ambaye ni mkuu wa vifaa wa Tigo amesema kwamba ofa hii ni jitihada za Tigo katika kuunga mkono serikali na wananchi katika kupinga bidhaa feki lakini pia katika kuimarisha mfumo wa pesa wa Tigo pesa.
Akizidi kufafanua bwana Zachariah anasema kwamba kwa wateja wa Tigo wanatakiwa kutembelea huduma ya wateja ambayo ipo katika maduka ya Tigo yote nchi nzima na kisha kuhakiki simu yake kama ni feki na iwapo itakuwa feki basi atapatiwa simu orijino ya Itel2100 kwa sharti moja tu la kujiunga na kifurushi spesheli cha dakika 350 sms 1000 na mb 250 ambacho ni shilingi 22000/=
Kwa kawaida simu hiyo ilikuwa inauzwa shilingi 30,000/= hivyo ofa hii itakupatia simu hii kwa shilingi 22000 na huku ukipata dakika sms na mb ambazo ndio thamani ya bei uliyonunulia.
Kwa taarifa zaidi tembelea ukurasa wa Tigo