Je, sabuni ya kuogea inaweza pia ikawa na kazi nyingine zaidi ya kutusafisha tu? Wengi wetu tumekuwa tukiugua malaria kwa kuona dalili kama: kupata homa kali, kutapika, kutokwa na jasho jingi, n.k. Njia nyingine ya kukulinda dhidi ya Malaria yagunduliwa.
Wanafunzi wawili walioshinda tuzo kwenye mashindano ya “Global Social Venture Competition (GSVC)”. Wanafunzi hao Moctar Dembele (22) kutoka Burkina Faso na Gerard Niyondiko (35) kutoka Burundi waliweza kushinda tuzo hiyo baada ya kuteneneza sabuni waliyoipa jina la “Faso Soap” ambayo ina uwezo wa kuzuia mbu wanaoambukiza Malaria (Anopheles).
Sabuni hiyo inayotenenezwa kwa ”Shea butter” na mafuta yatokanayo na majani ya Lemon pamoja na vitu vingine ambavyo wanafunzi hao hawakuviweka wazi.
Baada ya kutumia sabuni hiyo ina harufu ambayo itawafanya mbu waenezao malaria wasikuguse na kukufanya uwe umeepukana na kuugua malaria.
Ujio wa sabuni hiyo utasaidia wengi kutokana na kwamba gharama ya kununua sabuni ni ndogo kuliko gharama ya kununua dawa ya kutibu malaria. Pia, dawa hiyo itasaidia kushawishi watu wengi kutumia sabuni hiyo kusafisha miili yao pamoja na kujikinga na malaria.
Tuambie una mtazamo gani juu ya teknolojia hii?
Chanzo: CNN