fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Gari Teknolojia

Paris, Ufaransa – Magari yaliyoingia kabla ya 1997 Marufuku Barabarani

Paris, Ufaransa – Magari yaliyoingia kabla ya 1997 Marufuku Barabarani

Spread the love

Je unachukua hatua gani pale ambapo hali ya hewa inazidi kuwa mbovu katika jiji lenye magari maelfu kila siku barabarani? Piga marufuku yale yaliyozeeka, ndio uamuzi uliochukuliwa na serikali ya jiji la Paris.

gari uchafuzi wa hali ya hewa magari kabla ya 1997

Inafahamika wazi ya kwamba injini za magari yaliyochakaa yanatoa zaidi gasi chafu ukilinganisha na magari mapya na ya kisasa zaidi. Na ni kutokana na hili ndio maana serikali ya jiji la Paris limeona uhamuzi huu ni muhimu katika kuboresha hali ya hewa ya jiji hilo mashuhuri.

SOMA PIA  Tetesi: Apple kuanza kutumia OLED katika screen mwaka 2018

Kuanzia tarehe 1 mwezi wa saba mwaka huu, magari yote yaliyosajiliwa kabla ya 1997 na pikipiki zilizosajiliwa kabla ya mwaka 2000 hazitakuwa na ruhusa ya kutumika katika jiji hilo katika katika siku za kazi (weekedays), yaani Jumatatu hadi Ijumaa.

Mpango huu ni endelevu na lengo kuu ni kuhakikisha ya kwamba itafikia sehemu magari yenye umri wa zaidi ya miaka 10 hayatakuwa yanaruhusiwa kutumika kabisa katika jiji hilo.

SOMA PIA  Samsung yasitisha kuzalisha Galaxy J, sasa ni mwendo wa Galaxy A

Jiji hilo limejipanga kupanga magari katika makundi kulingana na sifa zake kwa mazingira, magari kama vile yanayotumia umeme na yale yanayotumia ‘hydrogen’ badala ya mafuta yatakuwa ya daraja la kwanza – yaani rafiki wa mazingira.

Hali ya hewa jijini Paris

Muonekano wa hali ya hewa kukiwa na ukungu uliosababishwa na uchafuzi wa hali ya hewa

Uamuzi kama huu ungechukuliwa katika mataifa kama yetu ya huku Afrika basi ungekuta ungeathiri zaidi ya asilimia 40% ya magari yote, lakini inasemekana kwa jiji la Paris ni takribani asilimia 10 tuu ya magari ndio yataathirika na uamuzi huu.

SOMA PIA  JIHUDUMIE: Huduma mpya kubatilisha muamala

Ila asimilia 10 hiyo ya magari inasemekana inachangia zaidi ya nusu ya gesi chafu yote inayozalishwa kutoka kwenye magari yanayotumika katika jiji hilo.

Kuna wakazi wengi ambao wamekasirishwa na uamuzi huo wakisema ni hatua ambazo wanaoathirika ni watu maskini, ambao wanaitaji kutumia magari hayo kwenye usafiri kwenda kazini n.k.

Vipi wewe unalionaje hili?

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania