Upo hapo? Mswaki wa dola 400 za kimarekani utakaokusafisha wakati huo huo ukiwa unakupa video za moja kwa moja (LIVE) za kinywani mwako kupitia simu yako.
Kampuni ya Onvi inayotengeneza miswaki ya umeme imeona labda kuna umuhimu wa wewe kupata kuona ni eneo gani hasa la meno unalisafisha katika mdomo wako na ndiyo maana wakaja na mswaki janja uliopewa jina la ‘Prophix Smart Video Toothbrush’.
Utumiaji wa miswaki ya umeme unakua taratibu na ata umoja wa afya za meno nchini Marekani (The American Dental Association) unashauri utumiaji wa miswaki ya umeme, wakisema ni bora zaidi kuliko miswaki ya kawaida tuliyoizoea.
Mswaki huo unakuja na kamera ya megapixel 10 yenye uwezo wa kuchukua video za kiwango cha HD (1080p).
Wanaamini kwa teknolojia hii basi utaweza safisha meno na maeneo mengine ya mdogo wako kwa ufanisi zaidi…umeona sehemu ina tatizo? Ipige picha na ukamuonesha daktari baadae! 🙂
2 Comments
Comments are closed.