Moja ya habari maarufu kwenye ulimwengu wa teknolojia ya magemu wiki hii ni kusitishwa kwa Playstation Mobile.
Playstation Mobile ni nini?
Playstation Mobile ni mpango wa kitengo cha magemu cha kampuni ya Sony wa kuwezesha magemu yanayochezeka kwenye vifaa vya mkononi vya Playstation Vita kuchezeka pia kwenye Androidi na iOS. Wakati Playstation Mobile ilipoanzishwa mwaka 2012, Sony waliona kwamba ukuwaji wa kuchezwa magemu kwenye Androidi na iOS ungeweza kuwapa fursa ya kukuza biashara yao ya magemu.
Kusitishwa kwa Playstation Mobile
Mpango wa kusitisha Playstation Mobile ulishatangulia kwa kusitishwa kwa huduma hii kwenye vifaa vya Androidi na sasa Sony wametangaza kwamba kuanzia Septemba 10, tovuti nzima ya Sony Mobile itafungwa na hivyo hata vifaa vya PS Vita navyo havitapata magemu mapya kutoka Sony Mobile. Hii haimanishi kuwa magemu yanayochezeka kwenye PS Vita pekee hayatakuwepo, magemu ya PS Vita pekee yataendelea kupatikana kwenye Playstation Store.
Je, ina maana kwamba Magemu kwenye Androidi yamefeli?
Kufungwa kwa mpango huu wa Playstation Mobile huenda unamaanisha kwamba kwa sasa Sony inaona magemu hayajakuwa na mvuto sana kwenye mfumo wa Androidi.
Si rahisi kusema kwamba Sony wana mtazamo huo ingawa ndivyo inavoonekana. Watu wengi ulimwenguni wanaaminika kuvutiwa zaidi na magemu ya vifaa vya mkononi kuzidi magemu ya TV. Mwaka jana, ripoti moja ya kampuni ya kuaminika ya Marekani ya utafiti ya Newzoo ilisema kwamba mfumo wa vifaa vya mkononi vya iOS ya Apple na Androidi pamoja huenda zikazalisha mapato ya kiasi cha dola za Kimarekani billion 7 (Trilioni 13 za Kitanzania) ambayo ni zaidi ya mapato ya magemu ya kwenye TV, ukizingatia ongezeko la watumiaji wa huduma za fedha za simu za mkononi.
Wewe unaonaje?
Jiunge nasi kwenye mitandao yetu ya facebook, instagram na twitter utuambie jambo hili limekugusaje?
Picha Na: alistdaily
No Comment! Be the first one.