Baba aliyepoteza mtoto kwa kosa la kuendesha huku akituma meseji, Brock Dietrich bado anamfikiria mwanae na nini angekua anafanya kipindi hichi. Kwa mfano hivi sasa alibidi awe anahitimu elimu yake ya juu.
Lakini mwanae (Sydnee Williams) huyo hawezi tena kamilisha malengo yake kwa sasa kwakua hayupo tena duniani. Sydnee alifariki katika siku yake ya kuzaliwa ya 18 kwa kosa la kuendesha gari huku akituma meseji katika moja ya barabara huko mjini Ohio.
Vijana wengi wametekwa na teknolojia, hili limewafanya wasijue maisha yao yakoje (yatakuaje) bila simu janja au wataishi vipi bila simu zao. Kutokana na kwamba tuko karibu sana na simu zetu, Elimu na kujua tuu havitaweza kupunguza hili tatizo la kuendesha huku kutumia simu lakini sheria ngumu zitatokomeza hili.
“Kinacho nisuta nafsi yangu na kuniuma zaidi, ni kwamba nilikua naendesha gari yangu huku nachezea simu yangu mbele yake” – Baba sydnee (39)
Dunia nzima inakubali kuwa kutuma meseji wakati wa kuendesha gari ni hatari, lakini jambo hilo limekua ni rahisi kulisema kuliko kuacha kulifanya. Ajali njingi zimetokea juu ya jambo hili ukiachana na hili lililo mpata Sydnee.
Utafiti umeshafanyika kwa madereva 904 kuhusu kutuma meseji au barua pepe wakati wa kuendesha gari, na majibu yalitofautiana na umri wa madereva hao
Zile Notification za mitandao ya kijamii zinazokuja pale juu ya simu, hasa za mitandao maarufu kama vile Twitter, Facebook na Instagram zinachangia kwa kiasi kikubwa sana watu kuangalia simu zo kila mara zinapotokea.
No Comment! Be the first one.