fbpx

Uwezo wa kupata jumbe zilizofutwa kabisa kwenye Gmail

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Tunafahamu vyema kuwa “Trash” ndio sehemu ambayo zile jumbe tunazozifuta kwenye barua pepe zetu zinakwenda huko na unapoamua kufuta kabisa maana yake ni kutoziona tena lakini ukweli ni kwamba uwezo wa kupata jumbe zilizofutwa upo!.

Nadiriki kusema kuwa unapofikwa na tatizo ndipo unapojua kufukiri vyema ili kuweza kutatua tatizo husika. Makala hii ya leo inanigusa moja kwani nilifuta kabisa ujumbe fulani ambao ni sikutakiwa kuufuta mpaka kazi yake itakapokuwa imekamilika na ndipo iliponibidi kufanya kila njia ili kuweza kuupata.

Google wana kipengele cha kutoa msaada (Google Help) na kiukweli ndio kilichonisaidia lakini haikuwa kazi rahisi mpaka kufikia hapo na ndipo baada ya muda nikaweza kuona hata zile jumbe ambazo nilizifuta miezi kadhaa iliyopita.

Ukibofya>>HAPA utapelekwa kwenye ukurasa ambao utajibu maswali kadhaa yatakayofanikisha kuweza kupata zile jumbe ambazo ulishazifuta kabisa kutoka kwenye kapu husika (trash).

kupata jumbe zilizofutwa

Maswali muhimu ambayo yataweza kurudisha zile jumbe ambazo hazipo kwenye akaunti yako (barua pepe).

Mbali na hapo njia ambayo unaweza ukaanza nayo ikiwa ya hapo juu ni ndefu kwako anza na hii ambayo inakupa uwanja upana zaidi kupitia kwenye kipengele cha “Search” kwenye Gmail ili kutafuta kile ambacho hukipati kwenye akaunti yako.

kupata jumbe zilizofutwa

Sio lazima ujaze kila kipengele ili kuweza kufanikiwa kupata kile unachokitafuta; unaweza ukajaza vipengele vichache tu kisha ukabofya “Search”.

Tafsiri ya hii makala ni kwamba kile ambacho tunakifahamu kuhusu barua pepe kutopatikana kabisa maara baada ya kuondoa kwenye “Kapu la uchafu” bado unaweza ukazipata hata mara baada ya miezi kadhaa kupita.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Udukuzi WhatsApp: Udukuzi mkubwa umefanyika kwa watumiaji wa WhatsApp
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.