Ukiangalia kwa siku tuu mtu unaweza pokea barua pepe nyingi sana za spam au zile ambazo huna mpango nazo (hazihitajiki). Unaweza ukawa unapokea namba kubwa sana ya barua pepe hizo lakini hivi haufikirii kuwa Inbox yako haitakiwa kupagha ghadhabu hiyo ya kupata zile usizokuwa na mango nazo?
Bila ya kushangaa hivi ushawahi kujiuliza pengine wewe mwenyewe ndio unaweza ukawa chanzo cha kupokea barua pepe nyingi zisizohitajika na zile za spam?
Lakini usiwe na shaka ngoja tuanzie kabisa katika chimbuko la hii kitu na kuona ni njia gani tunaweza tukaepukana na barua pepe za Spam.
– Fikiria Kabla Ya Kujiunga Ili Kupata Habari Fulani (Subscribe)
Kuna mambo ya muhimu ya kujiunga nayo kwa mfano TeknoKona. Inakupasa kufikiria kwa kina kabla hujajiunga na kitu chochote kwa kutumia barua pepe yako ili mradi upate taarifa zao. Kwa hiyo hapa kitu cha kwanza ni kujiuliza kama kweli utapata faida pindi utakapo toa barua pepe yako ili kupata habari au taarifa Fulani ambazo umeahidia
– Usiachie Barua Pepe Yako Wazi Kwa Jamii
Hii inategemea kama kazi yako inakuruhusu kufanya hivyo basi ni sawa tuu ingawa bado utapokea spam nyingi. Lakini vipi kama wewe kazi yako haikuruhusu, itakukosti sio?
Ndani ya mitandao ya kijamii yote (Facebook, Twitter n.k) badilisha ulinzi ili kuifanya barua pepe yako iwe ya siri (private). Yaani uweze kuiona wewe mwenyewe tuu. Na usiingize barua pepe yako sehemu yoyote ambayo unahisi inaweza ikawa wazi kwa jamii kuiona.
– Tumia Barua Pepe Ya Mbadala Au Mpya
Jinsi dunia ilivyobadilika siku hizi, kuna mambo mengi katika mitandao. Kuna vitu kama Forum mfano mzuri ni JamiiForum kwa Tanzania ambavyo huwa vinaomba barua pepe yako wakati wa kujiunga. Ni vyema ukatoa barua pepe ambayo huitumii mara kwa mara au ukatengeneza mpya kabisa. Hii itakusaidia kuiweka salama barua pepe yako ya kwanza kabisa. Hongera kwa wale wenye barua pepe zaidi ya moja kwa matumizi tofauti tofauti.
– Usijibu Barua Pepe Ambayo Ina Spam
Mara nyingine katika baadhi ya Barua Pepe tunazopokea tunaweza tukaamua kujitoa katika kupokea barua pepe hizo (unsubscribe) lakini mara nyingine wanaotutumia wanakuwa mbele yetu kiakili. Kwa kuchagua Unsubscribe watajua kwamba barua pepe yako inatumika mara kwa mara kwa hiyo watakutumia tena tuu. Cha muhimu hapa ni kuishitaki barua pepe unayopokea kama in spam (report) na vile vile kuifuta kabisa spam hiyo. Ukifanya hayo utakuwa umepiga hatua zaidi.
– Jitoe katika Kupata Habari (Unsubscribe) Kwa Usalama
Kama unajua kampuni au tovuti inayokutumia Barua pepe hizo basi ni salama kufungua ile link ya ‘unsubscribe’ ambayo mara nyingi huwa inakaa sehemu ya chini ya barua pepe iliyotumwa. Ukifungua link hiyo unaweza ukajitoa katika miongoni mwa watu ambao wanaweza kupata barua pepe hizo. Kama ni mtandao ambao ni wa uhakika basi watakuwa wameweka stepu zote za kujitoa na upokezi wa barua pepe zao katika inbox yako.