Japokuwa mwezi uliopita mkurugenzi mkuu wa ndege hizo alisema kuwa atapunguza kazi 4,000 tuu, bado imeonekana kuna haja ya namba hiyo kukuwa mpaka kufikia 8,000.
Kama inavyojulikana kuna makampuni mengi sana siku hizi ya ndege na kwa watu wa hali ya chini inayafanya yale ambayo yanatoza nauli kidogo kuwa na abiria wengi (tena kwa mkupuo) kuliko ndege zile zenye nauli za juu.
Boeing baada ya kuliona hilo waliahidi kupunguza baadhi ya rasilimali watu, kwa kujikita katika kupunguza kazi. Mwanzoni walisema wana mkakati wa kupunguza kazi japokuwa asilimia 10 katika kila kitengo mjini Washington.
Kupunguza nguvu kazi sio mkakati pekee ya Boeing. Mambo mengine ni kama vile kupunguza gharama za upatikanaji wa mali ghafi, kuongeza uzalishaji, kupunguza gharama zingine zinazohusiana na ufanyaji kazi nje ya muda wa kazi, usafiri na huduma zingine.
Boeing mpango wake ni kupunguza gharama kwa mabilioni ya dola za kimarekani ndani ya mwisho wa mwaka huu. Na kama njia hii haitafanikiwa basi huu mpango mzima unaweza ukajirudia tena mwakani.
“Njia ya haraka ya kupunguza gharama za uendeshaji ni kupunguza watu, hakuna njia mbadala juu yake” – Alisema Bw. Adam Pilarski
Tumeona katika makampuni mengi, ili kuliteka soko lazima uwe na huduma au bidhaa nzuri na kikubwa ni kwamba iwe na bei ya chini. Ili kuliwezesha hili inabidi kupunguza gharama zako za uendeshaji na kupunguza kazi ambazo sio za lazima. Pia ukibakia hapo hapo kwenye swala la kazi kumbuka kuna kazi zingine zinafanya na watu wengi wakati zilibidi zifanyike na mmoja tuu.